WANANCHI wilayani Rungwe mkoani Mbeya wameihoji ahadi
ya ujenzi wa barabara toka Ruangwa masoko,mwakaleli hadi katumba yenye kilometa
48 kwa kiwango cha rami iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania
Jakaya Kikwete mwaka 2005 wakati akiomba kura kwa wamanchi wa jimbo la Rungwe
magharibi.
Akizungumza na waandishi wa habari walipotembelea barabara hiyo kwa niaba ya
wananchi wengine Staford Mwaikape mkazi wa kata ya Bulyaga alisema Rais Kikwete
alipokuwa akiomba kura alitoa ahadi hiyo
kuwa atatengeneza barabara huyo kwa muda wa miaka mitatu lakini hadi anamaliza
muda wake hakuna kinachoendelea.
Alisema kuwa awali waliwahi kwenda kwa mbunge wao
Prof. David Mwakyusa kumshinikiza amkumbushe Kikwete kuitengeneza barabara hiyo
lakini walikwama baada ya mbunge wao kuhamia Dar,es,salaam huku akija kwa
mwaka mara moja na wao kukosa sehemu ya kupeleka malalamiko yao.
Aliongeza kuwa kutotekelezeka kwa miradi ya maendeleo
kwa nchi hii inatokana na baadhi ya viongozi kutosimamia misingi ya utawala bora
na kwamba wao kama wananchi wamepata somo kutokana na viongozi kutowajibika
katika shughuri za kijamii kama ilivyo kwa Rasi Kikwete.
“Aiingii akilini Rais kutoa ahadio alafu ashindwe
kuitekeleza huku mbunge nae ashindwe kumkumbusha na ndiyo maana viongozi wengi
wamekuwa wababaishaji kutokana na viongozi wao wakuu kutothamini misingi ya
utawala bora”alisema Mwaikape.
Mbunge wa jimbo la Rungwe Magharibi (CCM) Prof,David
Mwakyusa alipotakiwa kulizungumzia sakata hilo la kutosimamia masuala ya
kimaendeleo na kutomkumbusha Rais kutimiza ahadi hiyo huku akiishi
Dar,es,salaam na kuja kwa mwaka mara moja jimboni mwake kwa njia ya mtandao
hakuweza kujibu.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) wilayani humo
Ally Mwakalendile mbali na kukiri kuwepo na ahadi hiyo ya Kikwete alisema
upembuzi yakinifu umekwisha fanyika kwa kuanzia ujenzi wa kilometa 1.5 upande
wa Rungwe magharibi na upande wa mashariki kilometa 10.
“ni kweli Rais Kikwete aliahidi kuijenga barabara hiyo
na kwa kuwa ujenzi umechelewa wananchi wanahaki ya kuidai lakii hata kama
Kikwete akimaliza muda wake Rais ajae ataikamirisha hivyo wananchi wasiwe na
hofu juu ya ujenza wa barabara hiyo”alisema Mwakalendile.
Mkuu wa wilaya hiyo Chrispin Meela kwa upande wake
alisema kuwa wananchi wana haki ya kuidai barabara hiyo kwa kuwa Rais aliahidi
na kuwa kwa kuwa imechelewa wananchi wasiwe na hofu kwa kuwa tayari taratibu za
awal za ujenzi zimekwisha anza.
Kuhusu miradi mingine kujengwa chini ya kiwango na
mengine kuchakachuliwa Meela alisema tayari Serikali kupitia chama cha
mapinduzi imekwisha chukua hatu na tayari waliosababisha uchakachuaji huo
wameanza kuhojiwa.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment