Mwezeshaji Bi, Groria Mafule akiendele kutoa mafunzo katika ukumbi huo.
Mwezeshaji Bi, DorothyMbilinyi pia akitoa mafunzo kwa washiriki katika ukumbi huo.
Mratibu wa mafunzo hao kwa mkoa wa mbeya Alphonce Stima akiwa katika ukumbi wa mafunzo.
Washiriki wa mafunzo wakiwa darasani wakiwasikiliza wawezeshaji wakiwafundisha.
Mtandao wa jinsia, Tanzania Gender Networking Programme
(TGNP) unaendelea kutoa mafunzo kwa viongozi wa nyanja mbali mbali katika
ukumbi wa Malisho uliopo Uyole jijini mbeya yenye lengo la kuona umuhimu wa kushiriki chaguzi za serikali
za mitaa na uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2015.
Akizungumza na mtandao huu nje ya ukumbi huo mratibu wa
mafunzo hayo Alphonce Sitima amesema malengo ya mafunzo hayo ni kuwajengea
uwezo viongozi hao kuona umuhimu wa kushiriki kikamilifu katika chaguzi mbali
mbali za serikali.
Aidha Sitima amesema mafunzo hayo yamewalenga wanawake,
vijana na watu wenye ulemavu kwani makundi hayo yamekuwa mstari wa nyuma
kutokana na hali zao zilivyo na kujikuta wakipuuzwa pindi wanapotaka kutoa
maoni yao.
Stima ameongeza kuwa Mtandao huo umekuwa ukifanya kazi na
kituo cha haki za binadaumu kwa muda mrefu sasa kwa lengo la kuondoa dhana ya
unyanyasaji wa kijinsia ili waweze kujiamini na pindi inapotokea nasafi ya
uongozi waweze kuingia katika kinyang’anyoro hicho.
Kwa upande wao washiriki wa mafunzo hayo wamesema kupitia
mafunzo hayo wamepata uwezo wa kimaamuzi katika uchaguzi wa serikali za mitaa
hata katika uchaguzi mkuu wanaotarajia kufanyika mwakani.
“Sisi kama washiriki wa
mfunzo hayo kwanza tumenufaika kwa kiasi kikubwa sana na tumepata uwezo wa kuwa
na maamuzi katika jamii inayotuzunguka tofauti na siku za awali maana siku za
nyuma ilikuwa tofauti kidogo katika uelewa wetu ukilinganisha na sasa baada ya
kupata mafunzo haya” walisema washiriki hao.
Bahati Bukubilu ni mmoja kati ya washiriki katika kundi la walemavu
aliyetokea mbalizi jijini amesema kwa
upande wake amefurahishwa sana na mafunzo hayokwani hakuwai kushiriki katika
mafunzo kama hayo.
“mimi binafsi
nimefurahi sana kupitia mafunzo haya maana hii ndo mara yangu ya kwanza kupata
mafunzo kama haya hivyo nimetambua umuhimu wa kushiriki katika chaguzi mbali
mbali zinazotarajia kufanyika hapa ncini pia naiomba serikali kututengenezea
miundombinu katika sehemu mbali mbali hasa ofisi za serikali na mashirika
binafsi ili tuweze kuingia kwa urahisi maana serikali imekuwa ikituhaidi kuhu
kutengeneza miundombinu masipo kukamilisha” Alisema Bahati.
Hata hivyo mafunzo hayo yanatarajia kuendeshwa kwa muda wa
siku tatu ambapo leo ni siku ya pili tangu kuanza kwake na yanarajia kuisha september
24 mwaka huu.
Post a Comment
Post a Comment