GuidePedia

0


WANANCHI wa kitongoji cha Ibwe kijiji cha Mpunguti kata ya Luteba wilayani Rungwe mkoani Mbeya,wamelazimika kula nyama pori zikiwemo  panya buku,kicheche,nyani na lyakapenga kutokana na kupanda ghafra kwa bei za nyama ya ng’ombe na nguruwe.
Wakizungumza na mwandisi wetu alipowatembelea kijijini humo baada ya kupata taarifa ya tukio hilo walisema wameamua kwenda kuwinda wanyama pori na kura nyama zao baada ya bucha zilizopo kupandisha bei ya nyama bila kujali kipato duni walichokuwa nacho.
Mache Mwakalasi mkazi wa kijiji hicho alisema nyama ya ng’ombe na nguruwe zimepandishwa bei ambapo kwa kilio moja uuzwa kati ya Tsh,6,000 na 5,500 badala ya 4,000 ilivyokuwa awali na kupelekea kushindwa kumudu gharama hizo na kulazimika kuwinda wanayama pori na kuwafanya kitoweo.
“Sisi tumeamu kwenda porini kuwinda wanyama hao ili kuweza kupata mboga kwa lengo la kuzifanya familia zetu ziweze kupata mlo kutokana na kupanda kwa bei hizo huku serikali ikishindwa kuwadhibiti wafanyabiashara hao” alisema Mwakalasi.

Walisema kwa sasa wamekuwa wakishinda vichakani kuwinda wanyama hao na kuwa hawataenda buchani kununua nyama hizo hadi pale wafanyabiashara hao watakapo punguza bei.

Dr, Sangwe alisema madhara ya nyama hizo yanaweza kuwatokea kwa kuwa wanyama wengi hawajadhibitishwa kuliwa na kwamba hawafanyiwi vipimo japokuwa hakuna utafiti wa madhara yatakayowapata juu ya utumiaji wa wanyama hao.

Aliwataka wananchi hao kufuata ushauri wa maafisa mifugo pindi watakapo kuwatumia kwa vitoweo wanyama hao ili kukwepa madhara yatakayoweza kuwapata.

Mwisho.


                       Na, Lumemo blog 

Post a Comment

 
Top