Jengo la klabu cha pombe ambalo llgawanywa na chumba cha ofs ya kata hyo.
WANANCHI wa Kata ya Kawetele Tarafa ya Tukuyu mjini
wilayani Rungwe Mkoani Mbeya wanatarajia kufanya maandamano ya
amani hadi kwenye ofisi ya mkurugenzi wa Halmashauri hiyo kupinga hatua ya
ofisi yao kuwekwa kwenye kirabu cha pombe.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati
tofauti wamedai kitendo cha ofisi ya serikali kuwa katikati ya kirabu cha pombe
na kumbi za starehe kimeshusha hadhi ya mji wa Tukuyu ambao ndiyo makao makuu
ya wilaya hiyo.
Walida kuwa asilimia ishirini ya wananchi wa kata hiyo
ni walokole hivyo wanakosa kupata huduma za kiofisi kutokana na mazingira
mabaya ya kiofisi yalivyo hivyo hulazimika kupata huduma za kiofisi kwenye kata
za mbali kinyume na taratibu.
Wananchi hao ambao hawakutaka majina yao yatajwe katka vyombo vya habari walisema madai yao yakuomba ofisi kwa mkurugenzi mtendaji wa
Halmashauri hiyo Veronika Kessy yamegonga mwamba na kudai kuwa wamepanga
kufanya maandamano ya amani wakitaka kupatiwa ofisi.
Afisa mtendaji wa Kata hiyo Niklaus Kosama alikiri
kuwepo na hali hiyo na kudai kuwa yeye ameletwa kufanya kazi katika kata
hiyo na hana mamlaka ya kupinga ofisi kuwepo mahali hapo.
Anyimike Mwasakilali diwani wa Kata hiyo mbali na
kukiri kuwepo kwa hali hiyo pia alidai kuwa alipeleka maombi ya kupatiwa ofisi
kwa mwenyekiti wa Halmashauri na mkurugenzi wa halmashauri hiyo lakini
alikuwa akipigwa dana dana.
Alisema afisa utumishi wilayani humo alimueleza kuwa
amempa barua ya kuhama mtumishi anayeishi nyumba no,RDC/RHB/BLD/08 kuwa mwezi
wa 11 mwaka huu mtumishi huyo atahama na nyumba hiyo itafanyika kuwa ofisi ya
kata.
Waandishi wa habari walimulika hadi
kwenye nyumba hiyo kujiridhisha kana kwamba ni kweli mtumishi huyo wa
Idara ya maji kama kapewa barua ya kuhama,ambapo alikanusha kuwa hajawahi
kupewa barua ya kuhama na wala hata kwa mdomo.
Alfredy Mwakipiki mwenyekiti wa Halmasahuri hiyo kwa
upande wake alisema anachokijua ni kuwa wananchi wa kata hiyo walifanya
harambee ya kutaka fedha kwa ajili ya ununuzi wa uwanja na wao watawasapoti
pindi watakapo jenga hadi mtambaa wa panya.
Alisema Halmashauri ya Rungwe magharibi inakata 20 na
imekuwa ikishindwa kujenga kwa wakati ofisi za kata kutokana na bajeti
ndogo,hivyo suala la ofisi katika kata hiyo litapewa kipawa mbele pindi
wapatapo bajeti.
Na, Baraka Lusajo Rungwe
Post a Comment
Post a Comment