GuidePedia

0


Mwalimu wa shule ya msingi Misunkumilo kata ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa Osward Kapota Mpimbwe (33) amehukumiwa kwenda jela miezi sita kwa kosa la kutelekeza familia yake na kwenda kuishi na kimada

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa mahakama ya mwanzo Namanyere Baraka Stanley alisema kuwa mahakama hiyo imeridhika na ushahidi uliotolewa katika mahakama hiyo juu ya mwalimu huyo kuitelekeza familia yake ya watoto wawili na mke na kwenda kuishi na mwanamke mwingine na kuifanya familia hiyo kuishi katika mazingira magumu

Katika hukumu hiyo mahakama imeamuru mwalimu huyo pale atakapomaliza adhabu yake ya kifungo jela atalazimika kuitunza familia yake kama wajibu unanavyomtaka kama mzazi

Awali upande wa mashitaka uliieleza mahakama hiyo kuwa mwalimu huyo alimtelekeza  mke wake Lucy Malambugi ambaye amezaa naye watoto wawili kiasi cha kuifanya familia hiyo kuishi maisha magumu

Kutokana na kosa hilo mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa huyo chini kifungu cha sheria cha 167 sura ya 16 ambayo imeafanyiwa marekebisho mwaka 2002.

                                        Na, Lumemo blog


Post a Comment

 
Top