TIMU ya Taifa ya Tanzania (TAIFA STARS) imeweka kambi
wilayani Rungwe mkoani Mbeya ikiwa na wachezaji 33 chipukizi ambao
wanafanya mazoezi kwenye uwanja wa shule ya sekondari ya Msasani chini ya kocha
Oscar Koroso kwa lengo la kupata timu imara itakayoiwakirishi nchi katika
mashindano ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika kambi hiyo
iliyowekwe kwenye Hotel ya Landmark meneja wa timu hiyo Bonifas Clemens
alisema kuwa timu hiyo imeweka kambi wilayani humo wiki iliyopita na itakuwepo
kwa siku 60 ikiwa na wachezaji 33 makocha 3 kati yao mmoja ni wa makipa,daktari
1 na meneja 1.
Alisema wachezaji hao watachujwa na kubakia 15 ambao
wataungana na wachezaji 15 ambao hawajawahi kuchezea Taifa stars ambao
watachambuliwa tena na kubakia 15 watakaoungana na kocha mkuu wa timu ya Taifa
Stars ambaye atawaita wachezaji wa timu hiyo watakaoungana na wachezaji 15
watakaoshaguliwa.
Clemens aliongeza kuwa wachezaji ambao hawatachaguliwa
wataingizwa kwenye kumbukumbu ya Taifa kwa ajili ya kuongezwa pindi timu hiyo
itakapohitaji kuongeza wachezaji.
Naye kocha mteule wa Timu hiyo Oscar Koroso alisema
kuwa Chama cha Mpira wa miguu Nchini (TFF) kimeandaa mpango huu chini ya
udhamini wa Bia ya Kilimanjaro
kwa lengo la kupata timu nzuri ya Taifa itakayoweza kufanya vizuri katika
mashindano mbalimbali ya kimataifa na kuondokana na ukichwa cha mwandawazimu.
Koroso ambaye pia ni mwenyekiti wa chama cha makocha
wa mpira wa miguu nchini (TAFCA) aliendelea kusema kuwa mpango huu utaweza
kuleta mapinduzi ya mpira wa miguu hapa nchini na kuwa kinachotakiwa ni
watanzania kuwa na subira kwani mpango wa TFF unatija ndani yake.
Alisema kuwa wamechagua wilaya hiyo kwa ajili ya
kuweka kambi kutokana na hali ya hewa kuwa nzuri na watakuwepo kwa muda wa siku
60 na kwamba siku ya tarehe 4/05/2014 kutafanyika mchezo wa kujipima nguvu
unaotambulika na FIFA kati yao na timu ya Taifa ya Malawi kwenye dimba la
Sokoine na mwisho wa programmer hii ya siku 60 kutafanyika mchezo wa ujirani
mwema kati yao na Timu ya Taifa ya Burundi kwenye uwanja wa Taifa Jijini Dar es
Saalam.
Koroso aliongeza kuwa hali ya mazoezi inaendelea
vizuri huku wachezaji wakiwa na mudi na mazoezi hali ambayo inawapa hamasa wao
kama waalimu kuwapa mazoezi kwa utaratibu mzuri na kwamba katika wiki la kwanza
aliwapa mazoezi magumu na wiki hili la pili wanafanya mazoezi mepesa ya kucheza
mpira kwa makundi.
Aliongheza kuwa changamoto kubwa inayo wakabiri katika
mpango huo ni hali mbaya ya miundombinu ya barabara ya kutoka kambini hadi
kwenye Msasani ulipo uwaja huo ambapo gari la wachezaji limekuwa likikwama mara
kwa mara na kuleta usumbufu mkubwa,mvua zinazoendelea kunyesha wilayani humo
imekuwa ni maja ya changamoto lakini mambo yanaendelea vizuri.
Katibu wa chama cha mpira wa miguu (RUFA)wilayani humo
Joel Mpanda na mwenyekiti Frankylin Mwaisobo waliipongeza TFF kuandaa mpango
huo utakaoweza kuongeza tija kwa timu ya Taifa katika mashindano ya kimataifa
na kuondokana na usindikizaji katika mashindano.
Mkuu wa wilaya hiyo Chrispin Meela alisema kuwa ujio
wa timu hiyo ya Taifa kuweka kambi katika wilaya ya Rungwe kumeleta chachu
kubwa kwa vijana kuhamasika kutaka kuupenda mchezo huo na kuwa hali ya uchumi
utapanda kutokana na timu hiyo kununua mahitaji mbalimbali yanayouzwa kwa
wafanya biashara ambao wataongeza pato lao na wilaya kwa ujumla.
Alisema kuwa kamati yake ya ulinzi na usalama
imeboresha ulinzi katika hotel hiyo kwa lengo la kujihami na hali ya uvunjifu
wa amani unaoweza kujitokeza.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment