Afisa Mtendaji wa kijiji Malamba Emmanuel Wiliamu Gwimile, aliyesimama akifungua mkutano.
Mtendaji wa kijiji wa kata ya Rwiwa Zephania Mgaya aliyesimama akielezea baadehi ya changamoto wanakabiliana kwa lengo la kuzimaliza kaqtika kata hiyo.
Mwenyekiti wa kijiji cha malamba Nasibu Edson aliyesimama akizungumzia baadhi ya kero zilizopo katika kijiji hicho.
Diwani wa kata ya Rwiwa Alex Mdimilaje akihutubia kat.ika mkutano huo
B, Shali Kayeto mkazi wa kijiji cha malamba akiuliza swali katika mkutano.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza mkutano katika kijiji cha malamba.
Wananchi wa kijiji cha malamba kata
ya wimba wilaya ya Mbarali vijijini wametakiwa
kuacha tabia ya kutowapeleka watoto wao shule ya awali pamoja na darasa la kwanza.
Kauli hiyo imetolewa na Diwani wa
kata hiyo Mh, Alex Mdimilaje alipokuwa katika ziara yake ya kuangalia miradi ya
maendeleo pamoja na kuwaeleza baadhi ya ahadi zake alizozitekeleza katika kata
hiyo.
Mdimilaje amesema kuwa kumekuwa tabia
ya baadhi ya wazazi kutowapeleka watoto wao shule badala yake wamekuwa
wakiwaacha nyumbani na kuishia kufanya michezo isiyo na tija.
Aidha amesema faida ya
kuwapeleka watoto shule ni kukupa fursa
mzazi kufanya kazi za kimaendeleo pasipo kusumbuliwa na watoto hao kani walimu
watakao kuwa wanawafundisha wanataaluma ya kuishi na watoto.
Alex Mdimilaje ameongeza kuwa kuna
mradi wa umeme unaotarajiwa kuanza hivi punde na tayari fandi wameshaanza
kufunya uchunguzi wa kina ili kubani gharama ya kufikisha umeme huo katika
kijiji hichi.
Hata hivyo amesema katika kipindi cha
uongozi waake mpaka sasa amejitahidi kukamilisha miradi ya kimaendeleo kwa
asilimia kubwa tofauti na vile alivyoikuta wakati anaingia madarakani.
Kwa upande wake mtendaji wa kata hiyo
Zephania Mgaya amesema serikali inajitahidi kuongezza bnguvu katika miradi hiyo
ya maendeleo.
Aidha Mgaya amewataka wananchi kuwa
na imani serikali yao pamoja na kutekeleza maagizo yake yakiwemo ya
kujiandikisha majina kwaajili ya kupatiwa mashamba ya kulima mazao
yatakayowakwamua kiuchumi.
Hata hivyo Mgaya amesisitiza suala la
kujikinga na maambukizzi ya UKIMWI kwani ni ugonjwa ambao unamadhara makubwa
kwa wananchi na Taifa kwa ujumla.
Na, Lumemo blog.
Post a Comment
Post a Comment