Mtoto
mwenye umri wa miaka 12 mkazi wa
kitongoji cha kalulu kijiji cha kandete wilayani RUNGWE mkoani mbeya ameingia katika wakati mgumu baada ya kubakwa
na anosisye ligule mwenye umri wa
miaka 53 mkazi wa kijiji cha ipelo.
Wakiongea
na kipindi hiki mapema leo hii mashuhuda wa tukio hilo wamesema mnamo majila ya saa nne za asubuhi mtoto huyo
alijikuta akiingia katika wakati mgumu baada ya kujikuta akivamiwa
na mzee huyo katika eneo la makazi yao
na kwa kubakwa na kisha kuachiwa maumivu
makali katika sehemu zake za siri.
Hata
hivyo tukio hilo la kusikitisha na lililo acha simanzi kubwa kwa wakazi wa eneo
hilo limekuja kujitokeza baada ya binti huyo
kuachwa na wazazi wake katika makazi yao na huku wazazi wake wakiwa wameelekea katika shughuli zao za shamba ndipo kufumba na kufumbua mtoto huyo bila kujua hili wala lile
alijikuta akivamiwa na mzee huyo kwa
kuanza kufanyiwa kitendo hicho cha
kiunyama.
Hata
hivyo baada ya kilio kikubwa kusikika katika eneo hilo wananchi wenye hasila
kali waliwasili katika eneo hilo na
kushangaaa baada ya kumkuta mtoto huyo akifanyiwa kitendo hicho cha
kiunyama na mzee huyo ambapo bila kuvuta mda wananchi hao walimchukua
mtoto huyo na kumkimbiza katika kituo cha afya cha mwakaleli kwa matibabu zaidi.
Hata
hivyo kipindi hiki kilifanikiwa kuhojiana na
mwenyekiti wa kitingoji hicho
bwana elieza mwantimwa ambapo
amekili wazi kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa kwa ushirikiano mkubwa na wakazi wa eneo hilo waliweza
kumkamata mzee huyo na kumfikisha katika ofisi ya kata ya kandete.
Kwa
upande wa afisa mtendaji wa kata ya kandete
bwana HULUMA mwakyusa amekili
kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa mtuhumiwa amehifadhiwa katika mahabusu
ndogo ya mahakama ya mwanzo ya kandete
kwa mahojiano zaidi.
Pamoja
na hayo kipindi hiki kilifanikiwa
kuhojiana na mratibu kupitia
dawati la kupinga masuala ya ukatili wa kijinsinsia dhidi ya wanawake na watoto Diana
godwini ambapo amesema mpaka sasa wamejipanga
kumfikisha mahakamani mtuhumiwa huyo
kwa lengo la kujibia mashitaka
yanayo mkabili.
Adha godwini amewataka wanchi kuwafichua wahalifu wa matukio kama
hayo kwa lengo la kuweza kuwafikisha katika vyombo vya dora ikiwa ni pamoja na
kupungaza kasi ya maambukizi ya ukimwi
kwa wathilika wa vitendo hivyo.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa kituo cha
afya cha mwakaleli Dr , EDWINI MWAKISYA
amekili kubakwa kwa mtoto huyo na kuwataka wananchi kuacha tabia
ya kuwaogesha wathirika wa matukio kama hayo kabla ya kufikishwa katika
vituo vya afya kwani kwa kufanya hivyo kuna wawia ugumu wao kushindwa kupata ushahidi kwa haraka.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment