MHIFADHI wa wanyama pori katika hifadhi ya poli la
Lwafi wilayani Nkasi mkoani Rukwa Yohana Mateo(39 ) amefikishwa
katika mahakama ya wilaya Nkasi kwa kosa la kushawishi,kuomba na kupokea
rushwa kutoka kwa mfugaji ili asimchukulie hatua kwa kosa la kuchungia mifugo
ndani ya hifadhi
Akisomewa mashitaka na mwendesha mashitaka wa taasisi
ya kuzuia na kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Expediter Ngwembe mbele ya hakimu
mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila ni kuwa
mtuhumiwa huyo akiwa kama mtumishi wa serikali mnamo Marchi 2 mwaka huu
alimshawishi mfugaji Kashija Nsenga mkazi wa kijiji cha Kirando ampatie
Tshs,400,000 ili asi mchukulie hatua kwa kosa la kuchungia ng’ombe ndani ya
hifadhi.
Alisema kuwa baada ya hapo TAKUKURU waliweka mtego na
kumpatia mfugaji kiasi cha Tshs,100,000 na kuwa zoezi hilo lilifanyika
ndani ya ofisi ya mhifadhi mkuu wa wanyapoli wilayani Nkasi ambapo walifanikiwa
kumkamata mtuhumiwa na kumfikisha katika mahakama hiyo kujibu tuhuma
zinazomkabili
Mwendesha mashitaka huyo wa TAKUKURU aliiambia
mahakama hiyo kuwa mtuhumiwa huyo akiwa kama ni mtumishi wa serikali chini ya
wizara ya maliasili na utalii kwa kitendo chake cha kushawishi na kupokea
rushwa amekwenda kinyume na sheria kifungu No,15 (1)(2) ya mwaka 2007.
Mtuhumiwa kwa upande wake amekana shitaka na yupo nje
kwa dhamana chini ya wadhamini wawili kila mmoja ikiwa na thamani ya
Tshs,500,000 hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena aprili 10 mwaka huu.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment