Katika
jitihada za kuongeza kiwango cha
ufaulu kwa wanafunzi wa shule za msingi
na sekondari mkoani hapa ,
hivyo walimu wa shule hizo wameshauliwa kuwa
na ushilikiano kwa kufanya kazi kwa
pamoja kwa lengo la
kuongeza viwango vya ufaulu
kwa wanafunzi wote.
Hayo
yamesemwa na afisa maendeleo ya jamii katika
halmashauli ya busokelo
wilayani rungwe mkoani mbeya Agnes elikunda wakati
uzinduzi wa maadhimisho ya
sherehe ya wiki ya elimu iliyo fanyikia katika
viwanja vya shule ya msingi
lugombo wilayani hapa .
Ambapo
amesema ili wanafunzi waendelee
kufanya vizuri katika masomo yao hivyo walimu na wanafunzi hawanabudi
kuchukua hatua ya kushirikiana kwa pamoja
kwa kuwa na wivu katika kushindana kimasomo kwani kwa kufanya hivyo kutasaidia kiwango cha elimu kuendelea kusonga mbele
wakati wote.
Hata hivyo
elikunda ametumia fulsa
hiyo kuwataka wanafunzi wote katika
halmashaul hiyo juu ya kuepukana na vishawishi ambavyo vinaweza
kuhatarsha kupunguza kiwango cha masomo yao.
Kwa upande
wa walimu wakuu katika halmshauli
hiyo akiwemo JERMIAH ELESONI KAPANGA na Tumparege
mwaibingila wamesema ili kuboresha
elimu katika halmshauli hiyo serikali haina budi kuchukua hatua ya kuboresha vifaa vya ufundishaji pamoja na
miundo mbinu ya shule kama nyumba za walimu , na vyombo vya ufundi kwa
fani ya useremala.
Wamesema
endapo vitu hivyo vikitatuliwa mapema ufanisi wa ufundishaji kwa walimu utaongezeka kwa kiwango cha
juu ikiwa ni pamoja na ufaulu wa wanafunzi
kuongezeka kwa asilimisa kubwa
ukizingatia na hapo awari.
Uzinduzi
wa wiki ya elimu katika halmashauli ya busokelo umefanyikia katika shule ya
msingi ya Lugombo
ambayo ni miongoni mwa shule iliyo ongoza katika matokeo ya darasa la saba ikifuatiwa
na shule ya msingi Kisalala.
Post a Comment
Post a Comment