GuidePedia

0

Mganga mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya ya Ileje Kushoto mganga mkuu wakati mkuu wa wilaya ya Ileje Bi, Rosemery Senyamule



Mkuu wa wilaya Bi, Rosemery akikata utepe na kufungua rasmi uzinduzi huo.

Mkuu wa wilaya akianza kuwapatia chanjo watoto katika kampeni hiyo.

Mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Bi, Anna Mwakipesile akisoma taarifa fupi ya wilaya ya Ileje.

Mratibu wa huduma za chanjo mkoa wa mbeya Japhet Mhaye akisoma taarifa fupi ya mkoa wa mbeya.

Mganga mkuu wa mkoa wa mbeya Seif Mhina akisisitiza jambo katika uzinduzi huo

Mkurugenzi wa mtendaji wilaya ya Ileje Mussa Julius Otieno akiongea jambo katika uzinduzi huo.

Kaimu mganga mkuu wilaya ya Ileje Gerady Yubaha akisisitiza jambo katika uzinduzi huo.


Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbali mbali wakisubiri uzinduzi mkisha wapatiwe chanjo.




Baadhi ya wakazi wa wilaya hiyo waliohudhuria katika uzinduzi huo wakisubiri kupatiwa chanjo.

 

Wakazi wa mkoa wa mbeya wametakiwa kutumia fursa ipasavyo ya kampeni ya chanjo kwakuwapeleka watoto wao kupata huduma za chanjo ili kuwakinga watoto hao na maradhi yanayoweza kuwapata endapo kama watakosa kupata chanjo hiyo
.

Wito huo umetolewa jana na mkuu wa wilaya ya Ileje Bi, Rosemery Senyamule kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abassi Kandoro katika uzinduzi wa kampeni ya chanjo uliyofanyika katika zahanati ya kijiji cha ikumbilo kata ya chitete wilaya ya Ileje mkoani mbeya.


Bi, Rosemery Senyamule amesema mkoa wa mbeya umeadhirika na magonjwa yaliokuwa hayapewi kipaumbele.


“mkoa wetu wa mbeya umeadhirika na magonjwa ambayo yaliokuwa hayapewi kipaumbele mangonjwa hayo ni kama  vile minyoo, vikope, vichocho, usubi, matende, na ngiri maji, hivyo maambikizi ya magonjwa hayo yametapakaa katika wilaya zote kwa viwango tofauti” Alisema Rosemery Senyamule


Bi, Rosemery amesema serikali kupitia wizara ya afya na ustawi wa jamii imekuwa ikitekeleza mikakati mbali mbali ya kudhibiti maambukizi ya magonjwa hayo na mafanikio yameanza kuonekana ususani katika wilaya ya rungwe tathmini ya ugonjwa wa usubi iliofanyika mwaka 2013 ilionesha kuwa kiwango cha maambukizi kimeshuka kwakiwango kikubwa ukilinganisha na kiwango cha awali.


Akisoma taarifa fupi ya huduma za chanjo katika wilaya ya Ileje mratibu wa huduma za afya ya uzazi na mtoto Bi, Anna Mwakipesile amesema mwaka 2007na 2008 kulikuwa na wagonjwa wawili wa surua wenye umri wa chini ya mwaka mmoja, takwimu zinaonesha surua ilijitokeza kwa wingi katika kata ya mbebe na chitete.


Kufuatia hali hiyo wilaya imeendelea kufuatilia kwa ukaribu mwenendo wa ugonjwa huo ili kuutokomeza na kufikia septemba mwaka huu wamepeleka sampuli tano za watoto wanaoshukiwa kuwa na surua katika maabara kuu Dar es salaam na bado hawajapata majibu ya kimaabara.


Kwa upande wao wakazi wa wilaya hiyo wamesema wanaishukuru kwa kiasi kikubwa serikali kwakutambua na kuwajali wananchi wake kwakutilia mkazo huduma hiyo na kuizinduakampeni hiyo katika wilaya yao kwani kwakufanya hivyo imeleta msukumo mkubwa kwao wa kuwapeleka watoto wao kupata huduma hiyo ya chanjo.


Hata hivyo mganga mkuu wa mkoa wa mbeya Seif Mhina amewashukuru wakazi wa wilya hiyo kwakukujitokeza kwa wingi katika kampeni hiyo kwani kwakufanya hivyo inaonesha wanajali afya za watoto wao na kuwakumbusha wazazi wengine walioko majumbani wajitokeze kuwapeleka watoto wao badala ya kukaa majumbani kwani serikali yao inampango wa kuimarisha afya za watu wake.



                             Na, Lumemo blog










Post a Comment

 
Top