WATU watatu akiwemo mwanafunzi wa chuo cha uandishi wa habari mkoani Mbeya wamefariki dunia wakati wakiogelea katika fukwe za Matema beach katika ziwa nyasa liliopo wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja
wa shuhuda wa tukio hilo aliyenusurika na maafa hayo Godfrey Richard amesema
yeye Akiwa na rafiki zake wawili ambao ni madereva Bodaboda ambao ni Mark
Mwakipesile (17) na Noea Noha (16) wakazi wa kijiji cha Kawetele wilayani humo
na kumtaja mwingine aliyetambulika kwa jina moja la Happy mkazi wa kijiji cha
malindo wilayani humo aliyekuwa anasoma chuo cha uandishi wa habari mkoani
Mbeya na kusema kabla ya maafa
hayo aliambatana na wanafunzi
wengine mkoani hapa walioenda kuogelea katika ziwa hilo.
Amesema wao hawakujua kuwa ziwa
limechafuka waliingia kuoga wakati ziwa likiwa na mawimbi na kuwa yeye alikuwa
wa kwanza kukumbwa na kadhia hiyo na baadaye alifanikiwa kijiokoa huku wenzake
wakiwa wamezidiwa na harakati za
kuwaokoa ziligonga mwamba.
Amesema wananchi wanaoishi pembezoni mwa
ziwa hilo walifika baada ya kusikia mayowe ya kuomba msaada na kufanikiwa
kuwatoa watu hao wakati wamekwisha kata roho na kwamba waliwapeleka kuwahifadhi
katika hospital ya misheni ya matema beach iliyopo jirani na fukwe hizo na kuongeza kuwa baada ya hapo taratibu za
kuisafirisha miili hiyo ilifanyika na hivi sasa imehifadhiwa katika hospitali
Makandana iliyopo wilaya ya Rungwe huku ndugu wa marehemu wakiendelea na
maandalizi ya mazishi.
Mwenyekiti wa kitongoji cha kawetele
chini Syemu Melele amesema kitenda cha maafa kilichotokea kwa vijana hao
kimewasikitisha na kuwa walikwenda kuogelea bila kutoa taarifa kwa wazazi wao
na kuwa watafanya mikutano ya kukemea misafara ya kwenda matema beach pasipo
kutoa taarifa.
Post a Comment
Post a Comment