IMEELEZWA kuwa wilaya ya Rungwe mkoani Mbeya
imeshindwa kupanda kiuchumi kutokana na kushindwa kutumia fursa ya kuvitangaza
vivutio vilivyopo ambavyo havipatikani duniani kote vitakavyopelekea wilaya
hiyo ipande kiuchumi.
Kauli hiyo ilitolewa na katibu mkuu wa Christian and
Gospel Ministry (CGM)wilayani humo Watson Pamesa wakati wa makabidhiano ya
jengo la kufungia mitambo kwa ajili ya matumizi ya Redio Rungwe inayotarajiwa
kufunguliwa siku za hivi karibuni.
Makabidhiano hayo ya jengo la ngazi moja yalifanyika
baada ya uongozi wa Christian kuketi na wakuu wa idara kwenye ofisi ya
mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Veronika Kessy, ambapo mapendekezo na
muhtasari wa kikao hicho yatapelekwa kwenye kikao cha baraza la madiwani Agosti
26 mwaka huu kwa lengo la kujadiliwa.
Pamesa alisema waliiandikia halmashauri hiyo barua ya
kutaka kukodi jengo kwa matumizi hayo yenye kumb,RDC/E.1/117/97 ya
tare,07/8/2013 ambapo ilijibiwa na kusainiwa na kaim mkurugenzi wa halmashauri
hiyo Elias Sangi kwa barua yenye kumb,TKY/7.6/VOL.010/2014 ya Tar,30/05/2014
kuwa ombi lao limekubaliwa.
Alisema baada ya makubariano hayo siku ya alhamisi ya
tare,11/9/2014 walienda kuoneshwa jengo pamoja na mapendekezo ya ulipaji na
kuwa kinachosubiriwa ni maamuzi ya madiwani ambapo wataketi siku hiyo na kutoa
maamuzi.
Alivitaja vivutio hivyo ambavyo havipatikani Duniani
kote kuwa ni Vinyonga na Nyani wekundu waliopo mlima Rungwe,daraja la
mungu, ziwa ngozi na kisima ambacho maji yake hayajai wala hayakauki, mti
Rungwe ambao jina la wilaya limetokana na mti huo na unatibu magonjwa zaidi ya
45.
Alisema ujio wa redio hiyo utavitangaza vivutio hivyo
na kupelekea watalii kuzuru wilaya hiyo na kujionea maajabu ambayo hayapatikani
Duniani kote na kuwa wilaya hiyo itakuwa haishikiki kiuchumi kuliko ilivyo sasa
ambapo ni ya pili kutoka mwisho kiuchumi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Christian and Gospel
Ministry wilayani humo Amoni Mwakilomo mbali na kuipongeza halmashauri ya
wilaya hiyo kwa kuwaunga mkono pia amesema mchakato wa redio umefikia ukingoni
na sasa wanajipanga kuanzisha gazeti kwa lengo la kutoa huduma ya kihabari kwa
wanarungwe.
Post a Comment
Post a Comment