WANANCHI wilayani Rungwe
mkoani Mbeya wamemtaka mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wilaya
ya Mbeya mjini John Mwambigija (Mzee wa Upako) kugombea ubunge 2015 kuchukua
nafasi ya Prof,David Mwakyusa anayemaliza muda wake.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti walisema kuwa Jimbo
la Rungwe magharibi limekuwa na changamoto lukuki kutokana na sera
zisizotekelezeka za Chama Cha Mapinduzi hivyo wamemtaka mwambigija kuchukua
nafasi hiyo kwa kuwa wanaimani na sera za Chadema.
Wananchi hao ambao wengi wao
ni makada wa chama cha Mapinduzi ambao hawakutaka majina yao yatajwe katika vyombo vya habari walisema wilaya hiyo imekuwa ikiyumba kiuchumi ukilinganisha na
miradi Lukuki iliyopo na kuwa hali hiyo imetokana na usimamizi mbovu wa
viongozi waliopo.
Waliendelea kusema kuwa
kutokamilika kwa miradi ya maendeleo huku wakandalasi wakiitelekeza miradi hiyo
na wananchi wakikosa fursa ni ishara tosha ya kuwa viongozi waliopo wameshindwa
kusimamia miradi hiyo na wao kutaka kufanya maamuzi magumu 2015.
Walidai kuwa wamevumilia
muda mrefu wakidhani maisha bora kwa kila mtanzania yatatimia lakini
imeshindikana na sasa kumekuwa na maisha magumu kwa kila mtanzania na kuwa
wamemtathimini mwambigija kupitia Chadema ataweza kutatua matatizo ya jimbo
hilo.
Kwa upande wake Mwambigija
ambaye pia ni mwenyekiti wa hamasa nyanda za juu kusini Chadema alisema
anayaheshimu mawazo na ushauri wa wananchi na kudai kuwa atasubiri Baraka za
chama chake iwapo kitampatia ridhaa hata waangusha.
Aliongeza kuwa Chadema
kinaazina kubwa ya makada na sera nzuri zinazotekelezeka na nkwamba anasubiri
Baraka za chama hicho kama kitampitisha basi anauhakika kwa kushirikiana na
viongozi wengine ataupaisha uchumi ulioporomoka katika jimbo hilo lenye kata 26.
“nashukuru wananchi
kunitambua kuwa ni mchapa kazi na kuziamini sera na kanuni za Chadema
nawahakikishieni sitowaangusha kwa kuwa Chadema ni chama makini na kina watu
makini ukilinganisha na CCM,endeleeni kukiamini mabadiliko ya kweli
yanakuja”alisema Mwambigija.
Hata hivyo Mwambigija aliwatahadharisha
wananchi kuwa makini na makada wa Chama cha CCM wanaopita mitaani wakigawa vitu
mbalimbali kwa wananchi kutengeneza mazingira ya mtaji wa 2015 kuwa wawakatae
watu hao amedai hawataweza kuwatumikia kwa kuwa watakuwa wamepata uongozi kwa
pesa.
Post a Comment
Post a Comment