Wakazi wa kijiji cha lwanyo kata ya igurusi wilaya ya mbarali
mkoani Mbeya wamemtaka mwenyekiti wa kijiji hicho Laiton Mwakitwange kujiuzulu kwa kile kilichodaiwa kuwatukana matusi ya
nguoni wananchi wake pamoja na wajumbe wa serikali ya kijiji wakati wa mikutano
na nje ya mikutano.
Hayo yamesemwa na wajumbe wa serikali ya kijiji hicho pamoja
na wananchi katika kikao cha ndani kilichofanyika katika kanisa la (KKKT) mbele ya mkuu wa wilaya ya Mbarali Mh, Gulamu
Kifu.
Aidha wananchi hao walisea kuwa kutokana na matusi ya
mwenyekiti wao kuzidi wameona bora ajiuzulu kwani hata kama ataitisha mikutano
wananchi hawata shiriki kutokana na hali inayondelea kijiji hapo.
Hivyo wamesema kutokana na mwendendo huo itakuwa ni vigumu
kupata maendeleo kwa haraka kwani muda mwingi wamekuwa wakirumbana na kiongozi
huyo kufuatia matusi anayowatukana na kuwakashfu.
Kikao hicho kiliitishwa na mkuu wa wilaya hiyo mara baada ya
kupokea barua tofauti tofauti za malalamiko ya matusi pamoja na sehemu ya mradi
wa maegesho ya magari wa kijiji hicho kuhusu
mwenyekiti huyo ndipo mkuu wa wilaya huyo alilazimika kufanya kikao kwa lengo
la kumaliza tofauti hizo zilizopo kati ya mwenyekii pamoja na wajumbe na
wananchi.
Katika kujibu ya tuhuma hizo mwenyekiti huyo Laiton
Mwakitwange alikanusha tuhuma zinazomkabili na kudai wananchi wake waongo
wanamsingizia na kwamb hawai kumtukana mtu yoyote kwani yeye ndiye mara nyingi
amekuwa akisuluhisha matatizo ya watu anapotukanana hivyo isingeku rahisi yeye
anapiga vita hali hyo.
Kutokana na majibu hayo ya mwenyekiti ndipo mkuu wa wilaya
alilazimika kumwambia mwenyekiti
ajitazame mwenyewe kwani ni vigumu kuzingiziwa na wananchi wote hivyo
inaonyesha dhaili kuwa amehusika na tuhuma hizo na kuongeza kuwa siyo vema
kushindana na wapiga kura wake isipokuwa panapotokea tatizo wakaamu kulimaliza
kwa mazungumzo ya amani badala ya kurumbana kwani marumbano hayajengi bali
yanabomoa.
Baada ya mkuu wa wilaya kusema hayo ndipo mwenyekiti alikiri
na kuomba msamaha kwa wajumbe wake pamoja na baadhi ya wananchi waliyokuwepo
katika kikao hicho.
Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya baada ya kumaliza kikao
cha ndani wakaelekea katika mkutano wa
hadhra kwaajili ya kwenda kuzungumza na wananchi ambao hawakupata fursa
ya kuingia katika kikao hicho cha ndani.
Walipofika katika mkutano huo bado wananchi walishikilia
msimamo wao wa kumtaka mwenyekiti ajiuzulu kwani kwa matusi aliyoyatukana
katika mikutano iliyopita hastaili kuendelea kuwa mwenyekiti.
Hata hivyo mkuu wa wilaya aliamua kumsimamisha mwnasheria wa
wilaya ili aweze kueleza taratibu za kisheria zinazoweza kumuondoa madarakani
mwenyekiti huyo.
Na lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment