KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina la Musa Paulo (17)
mkazi wa kijiji cha Kacheche wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefikishwa katika
mahakama ya wilaya Nkasi kwa kosa la kumuoa mwanafunzi wa darasa la sita
Emiliana Kasamya (14)
Akisomewa
mashitaka mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Ramadhani Rugemalila
na mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi mkaguzi msaidizi wa polisi
Hamimu Gwelo alisema kuwa mtuhumiwa kwa makusudi aliamua kumuoa mwanafunzi huyo
huku akijua kuwa anatenda kosa kisheria
Alisema
kuwa jeshi la polisi lililpata taarifa za mtuhumiwa kuishi na mwanafunzi huyo
wa shule ya msingi Kacheche na ndipo walipoweka mtego na kwenda kumnasa
mtuhumiwa huyo akiwa anaishi kindoa na mwanafunzi huyo na kuwa kufanya hivyo
amevunja kifungu cha sheria No,4(2) cha sheria ya elimu ya mwaka 78
Mshitakiwa
amekana shitaka lake na amerudishwa rumande hadi kesi yake itakapotajwa tena
marchi 26 mwaka huu,na dhamana ipo wazi ila amekosa wadhamini
Wakati
huo huo kijana mmoja mkazi wa kijiji cha Mtapenda John Chulura (Ras)(35)
amefikishwa katika mahakama hiyo kujibu tuhuma zinazomkabiri za kulima nusu
ekari ya bangi
,mwendesha
mashitaka wa jeshi wa jeshi la polisi Hamimu Gwelo ameiambia mahakama hiyo kuwa
mtuhumiwa alikutwa anamiliki nusu ekari ya bangi iliyolimwa katika kijiji hicho
na kukamatwa na baada ya kuhojiwa ndipo alipofikishwa katika mahakama hiyo
Alisema
kuwa mtuhumiwa kutokana na kitendo chake cha kulima bangi amevunja sheria
kifungu namba 12(a) ya madawa ya kulevya ya mwaka 2002 na mtuhumiwa amerudishwa
rumande baada ya kukosa wadhamini hadi hapo kesi hiyo itakapotajwa tena march
23 mwaka huu
Post a Comment
Post a Comment