BODI ya mikopo ya serikali za mitaa hapa nchini
imeufanyia marekebisho muundo wake na kutengeneza muundo wa kibenki ambao
umeonekana kupendwa zaidi na wadau wengi kwa kuwa unaruhusu
kuwekeza na kuchangia mtaji kwa njia ya hisa na mikopo kutokana na misingi ya
usimamizi na uendeshaji wake ambayo ipo wazi.
Akizungumza
na madiwani wa halmashauri ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa mjumbe wa bodi hiyo ya
mikopo ya serikali za mitaa George malima Lubeleje alisema kuwa chombo hicho ni
muhimu sana kwa serikali za mitaa hivyo ni matarajio makubwa kwao kuwa
marekebisho ya muundo huo wa bodi ni kuwa na chombo makini cha kifedha
kitakachoziwezesha halmashauri hapa nchini kuendeleza miradi mbalimbali kwa
kuwa na uhakika wa kifedha.
Alisema
kuwepo kwa benki hiyo ya serikali za mitaa kutapelekea kuwepo kwa mtaji
wa kutosha kukidhi mahitaji ya wakopaji,kuzifanya halmashauri za wilaya
kuendeshwa kama kampuni ya kibiasshara(Business entities),kuwafanya viongozi
katika mamlaka za serikali za mitaa kuwa na mwamko zaidi wa kuibua shughuli za
maendeleo katika maeneo yao,kuongezeka kwa miukopo na viwango vya fedha
kuongezeka
Lubeleje
alisema kuwa lengo la serikali la kufanya marekebisho ya
muundo ni kutaka kuwa na chombo cha fedha cha serikali za mitaa
kilichoimarika katika Nyanja tofauti za kiutumishi katika Nyanja
mbalimbali za kiutaalamu,kifedha na katika technolojia ya habari na
mawasiliano,kuwa na chombo kinachojitegemea kwa kuwa na uwezo kiutendaji wa kusimamia
na kuendesha shughuli zake kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na kuwa na uwezo wa
kukidhi mahitaji ya mikopo katika ngazi zote za mamlaka ya serikali za mitaa.
Mjumbe
huyo wa bodi alifafanua kuwa licha ya hayo yanayofanywa na bodi hiyo ya mikopo
halmashauri kwa upande wake zina wajibu wa kuhakikisha zinasaidia katika
kuimarisha bodi ili itoe huduma kwa ufanisi zaidi na kutoa michango kwenye bodi
ya mikopo kwa mujibu wa sheria ikiwa ni pamoja na kuirejesha mikopo kwa wakati
Madiwani
kwa upande wao walionyesha kufurahishwa na chombo hicho na kudai kuwa wao kama
halmashauri hawakukifahamu na kuwa kama bodi hiyo ikitumiwa vizuri kuna
uwezekano mkubwa wa halmashauri yao kupiga hatua kubwa katika suala la
kujiletea maendeleo
Diwani
wa kata ya Nkomolo Sospeter Kasawanga alisema kuwa wao kama
madiwani hawakuitambua bodi hiyo ya mikopo katika serikali za mitaa na kuwa
sasa watabaki kujadili kwa kina suala hilo na kujiridhisha kama wanao uwezo wa
kukopa na kurejesha mikopo kwa wakati kupitia mapato yao ya ndani.
Mwenyekiti
wa halmashauri ya wilaya Peter Mizinga kwa upande wake
alisema kuwa halmashauri sasa itajipanga vizuri ili iweze kuona ni namna gani
wanavyoweza kuitumia bodi
hiyo katika kujiletea shughuli mbalimbali za kimaendeleo kupitia fursa zilizopo
kwenye bodi hiyo ya
mikopo.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment