SERIKALI mkoani Rukwa imesema kuwa upatikanaji wa maji
safi na salama katika mkoa huo ni asilimia 50 na kuwa kiwango hicho ni kidogo
sana na kuwa hari hiyo imesababishwa na jamii yenyewe kushindwa kuvilinda
vyanzo vya maji
Kauli
hiyo imetolewa na mkuu wa wilaya Nkasi mkoani Rukwa Idd Hassan Kimanta kwenye
kilele cha maadhimisho ya wiki ya maji kimkoa yaliyofanyika wilayani Nkasi
ambapo alimwakilisha mkuu wa mkoa Rukwa ambapo alisema kuwa lengo la
serikali ni kutaka kuwa ifikapo Septemba mwakani upatikanaji wa maji
ufikie asilimia 67
Alisema
kuwa ili kuyafikia malengo hayo ya serikali kunahitajika mshikamano wa pamoja
kati ya serikali na jamii husika kulinda vyanzo hivyo vya maji na kuhakikisha
miti haikatwi hovyo katika maeneo yote ambayo kuna hifadhi kubwa ya maji
Mkuu
huyo wa wilaya alifafanua kuwa serikali imekuwa ikitumia fedha nyingi katika
kutekeleza miradi mbalimbali ya maji kwa kushirikiana na wafadhili ikiwemo
benki ya dunia na kuwa miradi hiyo imekuwa ikizoroteshwa na uharibifu wa vyanzo
vya maji na kuwa hata kama kutakuwepo na miradi mingi kiasi gani kama vyanzo
vya maji havitalindwa ni kazi bure
Pia aliwataka viongozi wa kata ya Chala kuhakikisha
kuwa wanausimamia mlima Chala ambacho ni chanzo kikuu cha maji baada ya mlima
huo kukumbwa na majanga ya kuchomwa moto kila wakati na kuitaka halmashauri
kutunga sheria ndogo za kuwabana wachomaji moto mlima huo ikiwa ni pamoja na kuwafikisha
mahakamani watuhumiwa wa vitendo hivyo na kuona wanaadhibiwa
Mhandisi wa maji mkoani Rukwa Emmy George kwa upande
wake alidai kuwa licha ya wao kama serikali kujenga miradi mbalimbali ya maji
lakini pia wamekua wakiielimisha jamii mambo mbalimbali ya namna ya kuhifadhi
vyanzo vya maji,kulipia billi za maji kwa wakati ikiwa ni pamoja na mambo
mbalimbali ambayo jamii inatakiwa kuyafanya ili miradi hiyo iweze kuwa ni
endelevu
Kaimu katibu tawala wa mkoa Rukwa na ambaye pia ni mtoa huduma za menejimenti
ya serikali za mitaa Albinus Mgonya alisema kuwa hamashauri nyingi mkoani Rukwa
ziko nyuma sana katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maji kwa wakati na
kuwa sasa umefika wakati wa miradi ya maji kutekelezwa kwa kwa wakati ii
wananchib waweze kupata maji kwa wakati kama yalivyo malengo ya serikali
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment