KIJANA mmoja
aliyefahamika kwa jina la Sura Mbaya Lutemashimba (32) mkazi wa kijiji cha Maji
moto wilayani Mpanda mkoani Katavi amefikishwa katika mahakama ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa kujibu tuhuma zinazomkabili za
kujaribu kuua
Akisomewa
mashitaka yake mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi
Ramadhani Rugemalila mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi, mkaguzi msaidizi
wa polisi Hamimu Gwelo ni kuwa mtuhumiwa akiwa na wenzie watatu walimvamia
mwanamke mmoja Ng’washa Mondo (50) mkazi
wa kijiji cha Mtenga wilayani Nkasi na kumkatakata kwa mapanga kwa lengo la
kutaka kuua
Alisema
mtuhumiwa huyo akiwa na wenzie watatu baada ya kutekeleza hazma hiyo walikimbia
wakiwa na imani kuwa mwanamke huyo amekwisha kufa ambapo alizinduka baada ya
kufikishwa hospitalini
Mwendesha
mashitaka huyo wa jeshi la polisi alidai kuwa mtuhumiwa huyo sambamba na
wenzake walifanya uhalifu huo januari 7 mwaka huu nyumbani kwa mama huyo majira
ya saa 2 usiku na kukamatwa Februari 20 mwaka huu
Alisema kuwa
mtuhumiwa huyo amefanya kosa hilo chini ya kifungu cha 211 cha kanuni ya adhabu
sura ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 na kuwa mtuhumiwa ana kesi ya
kujibu
Mtuhumiwa
hakutakiwa kujibu lolote baada ya mahakama hiyo kutokuwa na uwezo wa
kuisikiliza kesi hiyo ambapo kesi itatajwa tena marchi 11 mwaka huu na
kurudishwa rumande
Upande wa
mashitaka uliitaka mahakama kutotoa dhamana kwa mtuhumiwa huyo kwa sababu
upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na pia watuhumiwa wengine watatu bado
hawajakamatwa
Wakati huo
huo mahakama ya wilaya Nkasi imemhukumu kwenda jela miezi sita au kulipa faini
ya Tshs,40,000 Martin Kipeta (32) mkazi
wa kijiji cha Isunta wilayani Nkasi kwa
kosa la kukutwa na bangi kilogramu 300 kinyume cha sheria
Mshitakiwa
alikutwa na bangi hiyo August 8 mwaka jana na kukutwa na kosa hilo chini ya
kifungu No,12 (d) sura ya 95 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002 ya sheria ya
kupambana na madawa ya kulevya
Mtuhumiwa
aliachiwa huru baada ya kulipa faini ya Tshs,40,000 baada ya mtuhumiwa kukiri
kufanya kosa hilo kinyume cha sheria
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment