Mchungaji wa Kanisa la Africa Mission Church wanakosali wazazi wa Marehemu akiongoza ibada ya Mazishi. |
baadhi ya Waombolezaji wakielekea Makaburini. |
Mwili wa Marehemu ukishushwa kaburini. |
Kaburi likifukiwa baada kukamilika kwa taratibu zote ambapo mwili wa marehemu ulizikwa katika makaburi ya Kijiji wanakozikwa Wananchi wengine. |
Kwa mujibu wa mila za kabila la Wanyamwanga vijana hawa walikuwa wakisiliba kaburi baada ya kumaliza mazishi. |
Ezekiel Richard Kamanga ambaye ni mwandishi wa Habari kutoka redio ya Bomba fm ya Jijini Mbeya akizungumza machache kwa wafiwa na wanakijiji kwa niaba ya Wanahabari wenzao ambao hawapo pichan. |
KATIKA hali ya kusikitisha Watoto wawili
kati ya Wanne ambao ni mapacha waliozaliwa kwa pamoja na mwanamke Aida Nakawala
Mkazi wa Kijiji cha Chiwanda Wilaya ya Momba Mkoani Mbeya wamefariki dunia kwa
ugonjwa wa Nimonia.
Watoto hao wamefariki kwa wakati tofauti
ambapo Mtoto wa Kwanza alifariki Nyumbani kwao baada ya kuugua ghafla ndipo
hali za wengine zilipoanza kutia shaka na kulazimika kuwakimbiza katika Hospitali ya Wazazi Meta
kwa matibabu zaidi
Hata hivyo baada ya kupokelewa kwa
watoto hao Watatu mtoto mmoja aliaga dunia baada ya kuchelewa kupata matibabu
kutokana na kubanwa na kifua na kusababisha kushindwa kupumua vizuri.
Hali za watoto wawili waliobaki
wanaendelea vizuri na matibabu na kwa mujibu wa Daktari anayewatibu amesema
taratibu za Hospitali hiyo ni kupokea watoto waliochini ya Miezi miwili lakini
hao wamezidi umri huo hivyo badala ya kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mbeya
wataendelea kuwepo Meta hadi hapo hali zao zitakapoimarika.
Baadhi ya wananchi na wauguzi katika
Hospitali ya Wazazi Meta wamesema sababu ya watoto hao kuugua ni kutokana na
kukosekana kwa uangalifu wa karibu katika malezi ya watoto hao ukilinganisha
na maisha ya vijijini kukosa watu wenye uelewa wa afya za watoto.
Wengine wameitupia lawama moja kwa moja
Serikali kwa kushindwa kuchukua hatua za haraka tangu watoto walipozaliwa ili
kujiridhisha na mazingira wanayopaswa watoto hao kuishi kwa kuwapatia msaada wa
karibu na ushauri wa kitaalamu.
Kwa upande wake Afisa Ustawi wa Jamii Mkoa
wa Mbeya, Thobias Mwalwego, alikiri kuwepo kwa urasimu katika Idara yao kwa
madai kuwa tangu watoto hao walipokuwa wamezaliwa walipata taarifa na kuchukua
hatua kwa afisa mmoja kufika kijijini na kuchukua picha zao.
Alisema urasimu unakuja kutokana na
Ofisi ya Wilaya na Mkoa kukosa fungu la dharula ambapo barua za maombi zote
hupelekwa makao makuu kwa Kamishna wa Ustawi wa Jamii ambapo Ofisi yake
huchukua muda mrefu kurudisha majibu kutokana na waombaji kuwa wengi.
Alisema kila ofisi katika Ngazi ya Mkoa
ingekuwa na fungu la Dharula kama ilivyo katika Ofisi zingine hali ambayo
ingeweza kusaidia kuepusha vifo vya watoto hao kutokana na kupatiwa msaada wa
ushauri na makazi rafiki kwa malezi ya mapacha wanaozidi wawili.
Na, Ezekiel Kamanga
Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment