Mwenyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo Mbeya mjini John Mwambigija aliyesimama katikati aliyevaa kofia upande wa kulia ni Samweli Ndoni Mwandishi wa habari wa Highlands fm
Baadhi ya wananchi waliokuwa wakimsikiliza mwenyekitti huyo kwa wakati akifanya uzinduzi huo
Baadhi ya wananchi wakimshangilia mwenyekiti huyo wakati wa uzinduzi.
Chama cha demokrasia na maendeleo mkoani mbeya kimewataka wananchi kuacha dhana ya kuamini kuwa vyama vyote vya siasa
ni viadilifu na vinalengo moja la kuwatumikia
wananchi kulingana na sera ya chama husika.
Hayo yamesemwa na mwenyekiti wa chama cha demokrasia
na maendeleo (CHADEMA) mbeya mjini John
Mwambigija alipokuwa akizungumza na mtandao huu katika uzindua wa kampeni za
uchaguzi wa viongozi wa vitongoji, vijiji na mitaa katika kitongoji cha
ilongoboto kijiji cha mpandapanda kata ya kiwira wilaya ya rungwe mkoani mbeya.
\
Mwambigija amesema chama cha Chadema kimekuwa na uwezo
wa kuwawajibisha viongozi wake wanaokwenda kinyume na sera ya chama, tofauti na
vyama vingine vimekuwa vikiwakumbatia viongozi wake ambao si waadilifu.
Aidha Mwambigija amesema dhana ya wananchi kuamini
kuwa wanapaswa kuchagu mtu na si chama ni kujinyima haki hao ya mingi. “wananchi wanatakiwa kuchagua chama chenye
uwezo wa kuwawajibisha viongozi wake ambao si waadilifu kwakufanya hivyo watakuwa wamepata
haki yao ya msingi, mimi nawaambia wananchi wa kijiji cha mpandapanda na Taifa kwa ujumla kama
mtachagua viongozi wa vyama vuinavyo wakumbatia viongozi wanaokula kodi yenu
kisha wanawakatetea basi mtaendelea kuchangishwa michango isiokuwa na tija kila
wakati” alisema Mwambigija.
Hata hivyo Mwambigija amesema chama cha Mapinduzi CCM
kimekuwa ni moja kati ya vyama vinavyowakumbatia viongozi wake ambao ni
mafisadi ikiwa wanafahamu wazi kuwa viongozi wake wanakula kodi za wananchi
pasipo huruma yeyote.
Akitolea mfano wa sakata la fedha shilingi bil. 321
zilizoibiwa katika akaunti ya Tegeta Escrow kwamba viongozi wa CCM ndio
wahusika wakubwa lakini jambo la kushangaza tuhuma hizo zimefunikwa funikwa
bila majibu sahii hivyo inaonesha kuwa chama hicho kinashindwa kuwawajibisha
viongozi wake.
Na, Lumemo blog.
Post a Comment
Post a Comment