SHIRIKA la The Strggler for Community Support Alliance
(SCSA),Limetoa misaada ya vifaa vya michezo vyenye thamani ya zaidi ya 1000,000
kwenye timu za mpira wa miguu kwa timu za Tarafa ya Ntebela na Unyakyusa kwa
lengo la kuinua viwango vya wachezaji wa mpira wilayani Kyela mkoani Mbeya.
Misaada hiyo ilitolewa jana na Mweyekiti wa Asasi hiyo katika
timu za New Fighter ya Ipinda ambayo ilipewa nyavu za magoli zenye thamani ya
Tsh,150.000,mipira sita yenye thamani ya 300.000,kwenye timu za
Kilombelo,Bwato,Ngyekye,Makwale Lyulilo na Ikombe huku timu ya Kyela Block 41
ilipewa jezi yenye thamani ya 200.000 pamoja na fedha taslim 100.000 kwa kila
timu.
Akizungumza mara baada ya kupokea misaada hiyo Katibu na
uenezi ambaye ni msemaji wa Timu ya New
Figher Imma Mwasimba alisema kuwa kwa muda mrefu timu yake ilikuwa na ndoto ya
kupata nyavu bila mafanikio na kwamba anaipongeza asas hiyo pamoja na uchanga
wake wameweza kuwa mfano wa kuigwa kwa mashirika mengine kwa kuwasaidia nyavu
pamoja na misaada mingine.
Alisema kuwa anawataka viongozi wa Asas hiyo waendelee na
moyo huo kwani watapiga hodi tena kuomba msaada pale watakapo hitaji na kwamba
asas hiyo imekuwa ikitoa misaada ya kijamii kila kona ya Wilaya hiyo na kuwapa
faraja kubwa wananchi wa Wilaya hiyo kwa misaada ya aina mbalimbali inayopewa
na wao kutumia kama ilivyo kusudiwa.
Edward Ntiandwale Timu Maneja wa Mababu sport club kwa upande
wake aliipongeza asas hiyo kwa misaada iliyoitoa kwa baadhi ya timu ikiwemo
timu yake iliyopewa mpira na fedha ambapo vijana wake hivi sasa wanajituma
mazoezini tofauti na ilivyokuwa awali na kuwa na wao wataonesha kiwango cha juu
katika cha uchezaji pindi ligi daraja la nne itakapoanza kama shukrani kwa
Shirika hilo.
Akizungumza mara baada ya kukabidhi misaada hiyo Mwenyekiti
wa Shirika hilo Kitaifa Dk, Abraham Mwanyamaki alisema kuwa Shirika lake ndiyo
kwanza limemaliza mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake na limesajiliwa ngazi ya
Taifa na linafanya kazi za kijamii nchi nzima na kuwa kwa kuanzia wameanza kutoa
misaada wilayani Kyela kwa kuwa ndiko yalipo makao makuu.
Alisema kuwa Timu zote zilizopewa misaada znatakiwa kutumia
misaada hiyo kama ilivyokusudawa ikiwa ni pamoja na kujituma kufanya mazoezi
ili waweze kutimiza ndoto zao za kupanda viwando na hatimaye kucheza ligi kuu
kama ilivyo kuwa kwa Gaudence Mwaikimba wa Azam aliyeanzia timu ya New
Fighter,Shadrack Nsajigwa aliyeanzia Maunt Rungwe na Kyela United na hatimaye
wakapanda viwango na kuchezea ligi kuu kwa ajili ya kujituma kwao.
Mwanyamaki aliongeza kuwa shirika lake lilianzisha ligi ya pambana
Cup itakayokuwa endelevu kwa kila mwaka lengo ni kuinua viwango vya
wachezaji chipukizi ambao badara ya kukaa vijiweni na kufanya mambo yasiyo faa
watakuwa wakijishughurisha na usakataji kabumbu ili waweze kupata ajira pindi
watakaposajiliwa na vilabu vikubwa.
Aidha Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa katika ligi ya Pambana
Cup ataboresha zawadi ili timu ziingie kwa wingi ili kuleta changamoto na
ushindani wa hali ya juu na kwamba anawaomba vijana wajikite katika michezo
hasa mchezo wa mpira wa miguu ili waweze kupata fursa zilizopo.
Post a Comment
Post a Comment