Hili ndiyo eneo la lililofyekwa miti na hii ndo miti iliyofyekwa na hawa ni baadhi ya wananchi wamaeneo hayo.
..............................................................................................................................................................
Wanachi wa
kijiji cha Itamboleo kata ya Itamboleo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
wameulamikia uongozi wa Kata na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya
kwa kutochukua hatua baada ya umoja kikundi cha wafugaji wa Matebete kuuza
ardhi ya kijiji kwa watu binafsi.
Mwenyekiti
wa kijiji Samwel Kaganga amesema kuwa eneo hilo lilitolewa na serikali kwa
ajili ya lanchi ya mifugo lakini badala ya kutumia eneo hilo kama ilivyokusudiwa
na serikali kikundi hicho kimefyeka baadhi ya maeneo na mengine kuyauza kinyume
cha sheria.
Taarifa
zimetolewa ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri lakini hakuna utekelezaji wowote
ambao umefanyika na kuwafanya wananchi waliokuwa wanamiliki mashamba hayo kuwa
vibarua ili waweze kujikimu na njaa.
Mwenyekiti
Kaganga ameiomba serikali kulipatia ufumbuzi suala hili ili kuepusha uharibifu
mkubwa wa mazingira unaofanywa na wafugaji kwa kukata miti hovyo ili kupata
mashamba ambayo huyauza kwa wafanyabiashara wakubwa wa Chimala na Mbeya.
Kwa upande
wake mkuu wa wilaya ya Mbarali Gulamhusein Kiffu ameahidi kulifuatilia suala
hilo ili kuepusha vurugu na pia kuzuia uharibifu wa mazingira ili kuepusha
Mbarali kugeuka jangwa.
Post a Comment
Post a Comment