Askari wanne
wa kikosi cha 44 KJ cha Jeshi la Wananchi kilichopo Mbalizi Mkoani Mbeya
wamesomewa maelezo ya mashahidi 13 dhidi ya kesi ya mauaji ya raia
inayowakabili katika mahakama ya wilaya ya Mbeya mbele ya Hakimu Mfawidhi
Gilbert Ndeuruo.
Akisoma maelezo
hayo Wakili wa Serikali Prosista Paul Minja amesema watuhumiwa hao ni pamoja na
Askari mwenye namba MT 101269 Omary Mwinchande[24],MT 101271 Rajab Mussa
Hamisi[23],MT 101263[23] Mussa Vuai Hassan na MT 99506 Richard Coster[24]ambapo
ilidaiwa kumuua Petro Sanga kwa kutumia kisu Novemba 18 mwaka 2012 majira ya
saa tatu usiku.
Imedaiwa
katika maelezo kuwa watuhumiwa walitenda kosa hilo kwa nia ya kulipiza
kisasi baada Askari mwezao aitwaye
Godfrey Katete kupigwa na raia eneo la DDC Mbalizi ambapo alijeruhiwa vibaya na
kulazwa ndipo watuhumiwa hao walimpiga marehemu na kumchoma kisu hadi kufikwa
na mauti.
Kosa hilo ni
kinyume cha sheria ya makosa ya jinai kifungu cha 199 cha kanuni ya adhabu sura
ya 16 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
Wakili wa
Serikali aliiambia Mahakama kuwa upande wa mashitaka utaleta mashahidi 13 ambao
ni pamoja na Rehema John,Bosco Choga,Happy Sanga,MT 100691 Said Malima,MT 62141
SGT Osia,MT 100620 Ramadhan Tofic,Amiri Sanga na Alinani Arden.
Wengine ni
pamojaT na Noah Malakesye,Maria Andulile,E 3843 SGT Greyson Askari wa
upekuzi,Mkaguzi wa Polisi Wambura na Daktari aliyefanyia uchunguzi mwili wa
marehemu.
Aidha Minja
amesema kuwa vidhibiti au vielelezo vitakavyowaslishwa kama ushahidi ni pamoja
na Taarifa ya Daktari aliyoifanyia uchunguzi maiti ya marehemu Petro Sanga
ambaye alikuwa ni mmachinga,Ramani ya eneo,Kisu kimoja na maelezo ya maonyo ya
watuhumiwa wote wane wa mauaji.
Hata hivyo
washitakiwa watatu wamesema kuwa wanao mashahidi wa upande wao ambao watawaleta
mahakamani na mshitakiwa wa kwanza amesema kuwa hana shahidi bali anategemea
daftari la zamu kwani anadai kuwa siku ya tukio alikuwa lindoni,ambapo Hakimu
amesema maelezo hayo atayatoa Mahakama kuu yeye hana mamlaka ya kusikiliza.
Baada ya
kupokea maelezo hayo Hakimu Ndeuruo amesema atapeleka maelezo hayo Mahakama kuu
ambapo ndiyo yenye dhamana ya kusikiliza kesi za mauaji kwani mahakama yake
haina uwezo wa kusikiliza ambapo aliahidi kuwapa nakala za maelezo ya mashahidi
katka kipindi cha muda mfupi ili wapangiwe siku ya kusikilzwa.
(Habari na Ezekiel Kamanga.)
Post a Comment
Post a Comment