GuidePedia

0

 Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu, wa pili toka mwisho wakati akikagua mradi wa uchimbaji wa Kisima cha Maji  uliofadhiliwa na Kampuni ya TBL  katika kituo cha Afya cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.



 Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,
Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, na pia ni mkaguzi wa ndani  Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.





Mganga wa Kituo hicho Dk. Gbson Mbaza alienyoosha mkono  alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.






KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL) imezitaka Halmashauri mbali mbali nchini ambako miradi mingi ya kijamii inatekelezwa kutokana na misaada ya Wahisani kutoa uangalizi ili iwe endelevu kwa manufaa ya wananchi ambao ndiyo walengwa.
Ombi hilo limetolewa na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Bia ya TBL, Doris Malulu,wakati akikagua mradi wa uchimbaji wa Kisima cha Maji  uliofadhiliwa na Kampuni hiyo katika kituo cha Afya cha Tunduma kilichopo Wilayani Momba Mkoa wa Mbeya.
Doris alisema maeneo mengi wanapeleka miradi ambayo Serikali ilitakiwa kuifanya ambapo baada ya kufanikisha miradi hiyo na walifadhili kuondoka miradi hiyo hufa kutokana na kukosekana kwa uangalizi toka Serikalini.
Alisema ili miradi iwe endelevu na imnufaishe mwananchi aliyekusudiwa ni vema suala la uangalizi likawa shirikishi kwa kila mtu ambapo itakuwa misaada kwa vizazi vijavyo na kwamba kampuni hiyo imelenga kituo cha Afya kwa kuwa ndiyo kimbilio la Watu wengi.
Aliongeza kuwa msaada wa kisima hicho unagharimu zaidi ya Shilingi Milioni 24, ambapo alisema TBL imetoa msaada huo ikiwa ni sehemu iliyojiwekea ya kurudisha fadhila kwa jamii kutokana na faida wanayopata kutokana na mauzo ya bidhaa zao.
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji mdogo wa Tunduma, Helen Kagamizi, aliishukuru Kampuni ya Tbl kwa msaada wa kisima cha maji katika Kituo cha Afya kwa kile alichosema Mji wa Tunduma unatatizo kubwa la uhaba wa maji.
Alisema mradi huo utakapoanza kufanyakazi utakuwa mkombozi kwa watu wengi hususani wagonjwa ambao ndiyo wahitaji sana wa Maji na kwa mujibu   Mkandarasi anayechimba kisima hicho anasema kinaweza kuzalisha lita 5000 kwa siku.
Naye Mganga wa Kituo hicho Dk. Gbson Mbaza alisema Tbl imetoa msaada mkubwa na muhimu katika sekta ya afya kwa sababu huduma hiyo inahitaji huduma ya maji kwa wingi kutokana na mahitaji ya usafi kwa wagonjwa na mazingira kuhitaji maji mengi.
Aliongeza kuwa maji hayo watayatunza vizuri ili yaweze kuwasaidia katika shughuli za kila siku za matibabu na wagonjwa kutokana na kukabiliwa na upungufu wa maji safi na salama kwa mji mzima wa Tunduma.

Post a Comment

 
Top