MGOGORO ulio
likumba kanisa la Moraviani Jimbo la Kusini Magharibi (Mbeya) baina ya waumini
walioungana na baadhi ya wachungaji dhidi ya Askofu wa jimbo hilo Alikisa Cheyo
umekwisha baada ya kufikishana mbele ya kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya.
Hatua hiyo
ilifikiwa Julai 16 mwaka huu baada ya mgogoro huo kudumu kwa zaidi ya mwaka
mmoja baina ya pande hizo mbili zilizotofautiana ndani ya kanisa hilo,
kufikishwa mbele ya kamati ya ulinzi na usalama, chini ya Mwenyekiti wake, Mkuu
wa Wilaya, Dk. Norman Sigalla.
Mgororo huo
umefikia katika hatua hiyo ikiwa ni siku tano tangu baadhi ya wachungaji
na waumini wa kanisa hilo ambao walikuwa na makufuri, na Minyororo
kuvamia na kisha kuteka na kufunga,lango kuu pamoja na milango yote ya ofisi
wakishinikiza kujiuzuru kwa Askofu huyo.
Taarifa za
kuaminika kutoka ndani ya kikaoo hicho kilicho fanyika katika ofisi za Mkuu wa
Wilaya na kudumu kwa zaidi ya saa tatu,pande zote mbili zinazo tofautiana
zilikiri wazi kwamba zilikiuka taratibu za kanisa na kuvunja katiba.
Akizungumza na
Mbeya yetu Blog moja wawajumbe walioshiriki kikao hicho na kuomba jina lake
liifadhiwa alisema kuwa kikao hicho kilikuwa na zaidi ya 30 na muafaka
ulifikiwa baada ya Askofu Cheyo kuonesha hekima na busara kubwa ambapo
alionyesha dhairi alikuwa na dhamira ya kweli ya kuliokoa kanisa hilo katika
migogoro na kwamba hekima hiyo ingeonyeshwa tangu awali wasingelifika hapo
walipofikia.
Akifafanua zaidi,
mpaka Askofu huyo kufikia hatua kutoa maneno ya hekima ni baada ya Mkuu wa
Wilaya, Dk. Sigalla kuonesha jinsi serikali ilivyochukizwa na mgogoro huo,
ambao ulionekana kuvuka mipaka na kuashiria uvunjifu wa amani katika Wilaya
yake na Mkoa kwa ujumla.
“Ni seme wazi
maneno ya Mkuu wa Wilaya kwamba serikali haiwezi kulinda fikra za waumini
waliochukia, ingawa itaweza kupeleka askari, lakini haiwezi kulinda mipango ya
kuchoma makanisa yalimgusa sana Askofu Cheyo wetu na mungu akamuongoza na
kuonesha busara na hekima juu ya suala hilo” alisema Mjumbe huyo.
Taarifa zinaeleza
kuwa Askofu Cheyo, ambaye ni baba wa kiroho ndani ya kanisa hilo,
alipopewa nafasi ya kueleza hali ya mgogoro huo na nini kifanyike,
alisema kimsingi, Mwenyekiti aliyesimamishwa Nosigwe Buya alifanya makosa ya
kiutendaji pekee.
Hivyo, ili aweze
kusamehewa na kurudishwa katika nafasi yake , anapaswa kuomba radhi kwa makosa
yake ya kiutendaji na ndipo Halmashauri Kuu iweze kumfikiria na hatimaye
kumrudisha kwenye nafasi yake.
Taarifa zaidi
toka ndani ya kikao hicho, zinadai kuwa Baada ya maneno hayo ya Askofu, ndipo
Mwenyekiti aliyesimamishwa Buya alisema kimsingi hana tatizo, lakini haamini
kama kauli hiyo ya askofu ina ukweli.
“Sina uhakika na
Askofu kwa kuwa amekuwa na tabia ya kubadilika badilika na kushindwa kusimama
kwenye kauli zake mara nyingi, hivyo kama atakihakikishia ukweli kikao hiki,
basi mimi sita kuwa na mengi zaidi ila isipokuwa lazima nimiweke masharti”
chanzo hicho kilimnukuu Mwenyekiti Buya.
Mara baada ya
kauli hiyo Buya alidaiwa kutoa masharti mawili, ambayo ni kutaka
Makamu Mwenyekiti Zacharia Sichone,ambaye ndiye mtendaji Mkuu wa shughuli zote
za kanisa na Halmashauri kuu kusambaza taarifa ya tume iliyoundwa
kuchunguza tuhuma za ubadhirifu fedha zaidi ya shiloindi milioni 200/ itolewa
na kusambazwa katika shirika zote 213 na idara zote za kanisa hilo.
Wakati sharti la
pili lililo tolewa na Mwenyekiti huyo aliye simamishwa ni kama taarifa
hiyo ya ubadhirifu itaoneka si za kweli basi aombwe radhi ili kosa la
kiutendaji lidhihirike, baada ya vinara hao kutoa masharti hayo,
yalionekana kuungwa mkono na wajumbe wote, na huyo ukawa ndo mwisho
na muafaka wa mgogoro huo.Mjumbe huyo alibainisha kuwa mbali na Busara za
Askofu na Mkuu wa Wilaya,alisema shukurani za pekee ni Mchungaji Hakimu
Mwandenuka kutoka Usharika wa Tunduma ambaye ni mmoja wa wajumbe pale
Mungu aliupo Muongoza kutumia vifungu vya kutoka biblia takatifu katika
kitabu cha Waebrania sura ya 12 , aya ya 14 hadi 15, maneno yaliyo wagusa
karibia wajumbe wote.
“Una jua maneno
aliyo yasoma Mchungaji Mwandemula yaliwagusa sana wajumbe nayo yanasomeka
‘Tafuteni kwa bidii kuwa na amani na watu wote, na huo ndio utakatifu ambao
hapana mtu atakayemuona bwana, asipokuwa nao, kwani shina la uchungu lisije
chipuka na kuwasumbua na watu wengi watatiwa unajisi kwa hilo”
.alisema Mjumbe
huyoKanisa hilo liliingia katika mgogoro huku wachungaji 20 na baadhi ya
waumini, wakiwemo wazee wa mabaraza ya kanisa hilo, wakipinga uamuzi uliofanywa
na Halmashauri kuu yaJimbo hilo huku Askofu Cheyo akitajwa kuwa kinara katika
uamuzi wa kumuondoa katika nafasi yake aliyekuwa Mwenyekiti Buya hatua iliyo
pelekea baadhi ya sharika kususa kupeleka sadaka ofisi kuu ya jimbo.
Post a Comment
Post a Comment