Wakili wa Serekali Mfawidhi mkoa wa Dodoma, Mhe Angaza
Mwaipopo akifafanua jambo wakati wa sherehe ya siku ya sheria mjini Dodoma leo.
Jaji Mfawidhi wa mahakama kuu kanda ya Dodoma, Mhe Crecensia
Makuru akizangumza jambo mbele ya watendaji na wadau wa mahakama wakati
sherehe za siku ya Sheria zilizofanyika leo.
Wakili wa kujitegemea Mhe Mary Munissi wa mkoani Dodoma
akielezea jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria yaliyofanyika
leo
Mahakimu, Mawakili na watendaji wengine wa
mahakama wakifuatila jambo walipokuwa kwenye maadhimisho ya siku ya
sheria yaliyofanyika leo Dodoma.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Dodoma akizungumza
jambo na Kaimu mkuu wa mkoa wa Dodoma ambaye pia ni mkuu wa mkoa wa Singida, Mh. Pasiseko Konne mara baada ya kumalizika shughuli za maadhimisho
ya siku ya sheria leo.
UCHELEWESHWAJI wa kesi nyingi mahakamani katika mahakama ya kanda ya Dodoma kunasababishwa na upungufu mkubwa wa majaji.
Hayo yalisemwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma,
Crecencia Makuru leo mjini humo wakati wa maadhimisho ya siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya mahakama kuu.
Alisema kuna upungufu mkubwa wa majaji ambao haulingani na
kesi zilizopo hali inayosabisha kuzolotatesha mienendo ya kesi mbalimbali.
Crecencia alisema majaji katika kanda ya Dodoma ni
wachache kulingana na kesi zilizopo ambapo
hadi kufikia Desemba 31, 2013 kulikuwa na jumla ya mashauri na 1364 na kuna
majaji wawili tu.
Alisema ''idadi ya kesi ni kubwa mno kwa majaji wawili
hii inachangia kwa kiwango kikubwa kesi kutosikilizwa na kutolewa maamuzi kwa
wakati, upo umuhimu wa kuongeza majaji ili
kuwe na uwiano wa masharti yaliyopo'',
Aidha alisema Mahakimu ni wachache huku mahakama
nyingi za wilaya zina hakimu mmoja mmoja licha ya kuwa na mashauri mengi na tatizo linakuwa
kubwa pindi mahakimu hao wanapougua, kuuguliwa au kwenda likizo.
Aliongeza kuwa mahakama nyingi za mwanzo hazina mahakimu wa
kudumu, mahakama hizo hutembelewa na mahakimu kutoka vituo vingine hali ambayo
husababisha ucheleweshaji wa haki kwani mahakimu hulazimika kusafiri umbali
mrefu na wakati mwingine miundombinu huwa ni mibovu..
Jaji huyo alibainisha
kuwa sasa posho za washauri wa mahakama zimeboreshwa kutoka Sh.1,500 hadi
kufikia 5,000 kwa kila shauri litakalohitimishwa.
Alisema licha ya changamoto mbalimbali zinazoikabili
mahakama kuna mikakati ya kutatua
changamoto hizo ikiwemo kuondoa mashauri, kesi zote zenye umri zaidi ya miaka
miwili, kuboresha takwimu za mashauri, kesi zilizopo mahakamani, kuboresha na
kusimamia masjala pamoja na ukaguzi wa mara kwa mara.
Post a Comment
Post a Comment