WATU
WATATU WA FAMILIA MOJA WALIOTAMBULIKA KWA MAJINA YA STEVEN MWAIJOMBE
(35) BABA WA FAMILIA, ESTER KIBONA (25) MAMA WA FAMILIA NA MTOTO WAO
EDGAEL STEVEN MWAIJOMBE (02) WOTE WAKAZI WA SOGEA WALIFARIKI DUNIA BAADA
YA KUANGUKIWA NA UKUTA WA NYUMBA YAO WAKIWA WAMELALA. TUKIO HILO
LILITOKEA MNAMO TAREHE 07.02.2014 MAJIRA YA SAA 04:45HRS USIKU WA
KUAMKIA LEO HUKO ENEO LA SOGEA KATA NA TARAFA YA TUNDUMA WILAYA YA MOMBA
KUFUATIA MVUA KUBWA ZINAZOENDELEA KUNYESHA MKOANI MBEYA. MIILI YA
MAREHEMU IMEHIFADHIWA KATIKA KITUO CHA AFYA TUNDUMA. KAMANDA WA POLISI
MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI AHMED Z. MSANGI
ANATOA POLE KWA NDUGU NA MAJIRANI WA FAMILIA HII KUTOKANA NA JANGA
HILO.
WATU 07 WAKAMATWA NA JESHI LA POLISI MKOANI MBEYA WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAWASHIKILIA WATU 07 WAKIWA NA POMBE HARAMU YA MOSHI [GONGO] UJAZO WA LITA 11/2.
KATIKA MSAKO ULIOFANYWA MNAMO TAREHE 06.02.2014 MAJIRA YA SAA 19:30HRS
USIKU HUKO MWANJELWA NA MAFIATA JIJI NA MKOA WA MBEYA EMANUEL MBWETE
(27) MKAZI WA MAKUNGURU AKIWA NA WENZAKE 05 WALIKAMATWA WAKIWA
WANAKUNYWA POMBE HARAMU YA MOSHI. PIA KATIKA MSAKO MWINGINE HAMASHA
PAULO (25) MKAZI WA FOREST MPYA ALIKAMATWA AKIWA ANAKUNYWA POMBE YA
MOSHI. TARATIBU ZA KUWAFIKISHA MAHAKAMANI WATUHUMIWA ZINAFANYIKA.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI MWANDAMIZI WA POLISI
AHMED Z. MSANGI ANATOA WITO KWA JAMII HASA VIJANA KUACHA MATUMIZI YA
POMBE HARAMU YA MOSHI KWANI NI KINYUME CHA SHERIA NA NI HATARI KWA AFYA
YA MTUMIAJI.
Signed by:
[AHMED Z. MSANGI – SACP]
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment