MAHAKAMA ya
wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kwenda jela miaka miwili afisa mtendaji wa
kata ya Mtenga Damas Ismail (35) kwa kosa la kumuibia mwajiri wake ambaye ni
halmashauri Tshs,5050,000 ambayo yalikusanywa kama ada ya viwanja
Kwa mujibu
wa mashitaka yaliosomwa mbele ya mahakama hiyo na mwendesha mashitaka wa polisi
mkagaguzi msaidizi Hamimu Gwelo ni kuewa mtuhumiwa akiwa kama mtumishi wa
halmashauri alimwibia mwajili wake kiasi hicho cha fedha mwaka 2011 baada ya
kuhamishiwa ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Namanyere akitokea kata ya Mtenga
Alisema kuwa
mtuhumiwa huyo kwa makusudi aliamua kuziiba fedha hizo huku akijua kuwa ni mali
ya mwajili wake ambaye ni halmashauri ambapo alifanya kosa hilo katika nyakati
tofauti ambapo katika mahakama hiyo alikuwa anatuhumiwa kwa makosa matano
ambapo yote alikua akimuibia mwajili
wake
Hakimu mkazi
mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila baada ya kuridhishwa
na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka
pasipo kuacha shaka yoyote alimtia hatihani mtuhumiwa huyo kwa kumpeleka
jela miaka miwili na akitoka atalazimika kumlipa mwajili wake kiasi hicho cha
fedha Tshs,5050,000
Alisema kuwa
mtuhumiwa anatiwa hatiani chini ya kifungu namba 258 na 270 sura ya 16 ya
kanuni ya adhabu iliyofanyiwa
marekebisho mwaka 2002
Awali upande
wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili liwe ni
fundisho na kwa watumishi wengine wenye nia ya kutaka kufanya kosa kama
hilo,ukichukulia hivi sasa watumishi wengi wa serikali wamekuwa wakituhumiwa
kufanya vitendo kama hivyo vya uhalifu.
Post a Comment
Post a Comment