Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
itakutana kwa ajili ya kikao cha dharura, Februari 14, mwaka huu, jijini Dar es
Salaam.
Katika kikao hicho, Kamati Kuu itajadili na kufanya uteuzi wa
mwisho wa jina la mgombea ubunge wa CHADEMA katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la
Kalenga, mkoani Iringa, unaotarajiwa kufanyika Machi 16, mwaka huu.
Kikao hicho kitafanya uteuzi wa mwisho, baada ya mchakato wa
ndani wa kumpata mgombea ubunge wa Jimbo la Kalenga kwa tiketi ya CHADEMA, kuwa
umepitia hatua za awali, ambazo ni pamoja na watu wote wenye nia ya kugombea,
kuchukua fomu za uteuzi wa ndani tangu Februari 5-10, mwaka huu.
Kama ilivyoelezwa kwa umma kupitia vyombo vya habari,
Februari 6, mwaka huu, fomu hizo zilitolewa katika maeneo matatu, Ofisi za
Makao Makuu ya Chama, Dar es Salaam, Ofisi za Jimbo la Kalenga.
Jumla ya watu 16 waliweza kuchukua fomu za kuwania uteuzi huo,
ambapo hadi siku ya mwisho, watu 13 waliweza kurejesha fomu zao na kupita
kwenye mchakato wa kura za maoni, zilizofanyika Februari 12, mwaka huu.
Imetolewa leo Februari
13, 2014, Dar es Salaam na;
Tumaini Makene
Ofisa Mwandamizi wa Habari- CHADEMA
na Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment