Rais Kikwete kabla ya kuanza matembezi leo asubuhi eneo la Soweto Jijini Mbeya. |
Mwenyekiti wa CCM Taifa akisalimiana na Makamu Mwenyekiti mara kabla ya kuanza matembezi ya mshikamano leo asubuhi. |
Rais Kikwete akiwasili katika eneo la Soweto kwa ajili ya kuanza matembezi ya Mshikamano. |
Baadhi ya Waandishi wa Habari wakiwa katika magari mawili ya Polisi wakichukua matukio wakati wa matembezi ya mshikamano leo asubuhi |
Rais Kikwete na Mwenyekiti wa CCM Taifa akizungumza na wananchi mara baada ya kumaliza matembezi ya mshikamano katika Bustani ya Jiji la Mbeya leo asubuhi. |
MWENYEKITI wa chama cha Mapinduzi CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete leo
ameongoza matembezi ya mshikamano Jijini Mbeya kwa kutembea umbali wa
kilomita 2 kutoka eneo la Soweto hadi Uwanja wa Sokoine.
Matembezi hayo ya mshikamano yameambatana na maadhimisho ya miaka 37
tangu kuzaliwa kwa chama hicho Februari 5 1977 ambapo kitaifa
yanafanyika mkoani Mbeya katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine leo
mchana.
Rais Kikwete ambaye aliambatana na baadhi ya viongozi wa Chama na
Serikali wakiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Philip Mangula, Katibu Mkuu
Abdulrahman Kinana, Waziri wa Rais Kazi Maalum Prof Mark Mwandosya,
Waziri wa Uchukuzi Dkt Harrison Mwakyembe,Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Mbeya ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika Godfrey
Zambi, Naibu Waziri wa Fedha Mwigulu Mchemba,Mkuu wa Mkoa wa Mbeya na
viongozi wengine wa ngazi ya Mkoa na Taifa.
Matembezi hayo ambayo yalianza majira ya saa 1:00 asubuhi yameishia
katika Bustani ya Jiji la Mbeya iliyopo karibu na Uwanja wa Kumbukumbu
ya Sokoine ambapo Rais Kikwete aliungana na mamia ya wananchi kutembea
bila kuchoka.
Katika maandamano hayo Rais Kikwete aliwachukua watoto wanne na
kuongozana nao hadi mwisho wa matembezi ambapo baadaye aliwataka
wanausalama kuchukua majina ya watoto hao na kumkabidhi.
Tofauti na ilivyokuwa katika miaka ya nyuma eneo la Soweto,Kabwe na
Mwanjewa ambako mara nyingi kumekuwa na historia ya vurugu, baadhi ya
wananchi na wafanyabiashara wa maeneo hayo walijitokeza kwa uchache na
kupungia mkono matembezi hayo bila vurugu zozote.
Post a Comment
Post a Comment