GuidePedia

0
KIJANA mmoja aliyejulikana kwa jina la Charles Lutonja  (19) mkazi wa kijiji cha Kipundukala kata ya Namanyere wilayani Nkasi mkoani Rukwa amefikishwa katika mahakama ya wilaya Nkasi kwa kosa kuua mtoto wake Hollo Lutonja (1)
Akisomewa mashitaka  na mwendesha mashitaka mashitaka wa jeshi la polisi wilayani Nkasi Hamimu Gwelo mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila ni kuwa mtuhumiwa alimuua mtoto wake huyo februari 8 mwaka huu baada ya kutokea ugomvi wa kindoa kati yake na mkewe  Bi.Lutenganija Lutoja
Alisema kuwa mnamo siku ya februari 8 majira ya saa 3 za asubuhi mtuhumiwa alianza kumpiga mkewe kwa kutumia fimbo na pembeni alikuwepo mtoto wao mchanga na baada ya mke kuikwepa fimbo ile ilikwenda kumpiga kichwa mtoto wao Holo Lutoja na kupelekea mauti baada ya kufikishwa katika hospitali teule ya wilaya Nkasi na kupoteza maisha muda mfupi
Mwendesha mashitaka huyo wa polisi alisema kutokana na hilo mtuhumiwa alitenda kosa  chini ya kifungu cha 196 cha kanuni ya adhabu  sura ya 16 kama ilivyofanyiwa marekebisho mwaka 2002
Mtuhumiwa hakutakiwa kujibu lolote katika mahakama hiyo kwa sababu haina uwezo wa kuisikiliza kesi hiyo na alirudishwa rumande hadi kesi hiyo itakapotajwa tena Februari 27 mwaka huu

Post a Comment

 
Top