WANANCHI wa Vijiji vya Ndoa,liunji,Kimata na Makaonde kata ya
Makaonde Tarafa ya mwambao wilayani Ludewa mkoani Njombe wameulalamikia uongozi
wa vijiji hivyo pamoja na kata kwa ujumla kwa kushindwa kusimamia na
kutelekeleza shughuri za maendeleo ya kata hiyo kwa zaidi ya miaka nane.
Wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti
katika walipotembelewa katika vijiji hivyo walisema kuwa wamekuwa wakijitahidi kuchangia nguvu kazi
zao katika shughuri za maendeleo lakini serikali za vijiji hivyo imekuwa
ikikwamisha shughuri za maendeleo kwa kushindwa kusoma mapato na matumizi huku
jitihada za ujenzi wa miradi ikisuasua.
Alfan Ngoye na Wilson Kaluwa kutoka kijiji cha Makonde
walishusha tuhuma kwa Diwani wa kata ya Makaonde Chrispin Mwakasungura (MWENDAKOTE)pamoja
Mwenyekiti wa kijiji hicho Sosten Haule(KISADO)kuwa ndiyo kikwazo cha maendeleo
katika kata hiyo kwa kushindwa kusimamia miradi kadhaa iliyotengewa bajeti na
Serikali.
Waliitaja miradi ambayo imetengewa bajeti na wao kushindwa
kusimamia kuwa ni madaraja ambayo baadhi yamejengwa chini ya kiwango,ukarabati
wa kituo cha afya ambacho kilitengewa fedha zaidi ya million 20 lakini
kilichofanyika ni kupaka rangi tu na fedha hazijurikani zimetumika kiasi gani
na kuwa vibarua waliokuwa wakisaidia ujenzi hawajapata stahiki zao.
Waliutaja mradi mungine kuwa ni ujenzi wa nyumba mbili za
waalimu ambao haujakamilika wakati Serikali ilitoa pesa na wananchi kuchangia
nguvu zao kwa kuchangia matofali lakini hawajui ni lini ujenzi huo utakamilika
na kuwa kutokana na hali hiyo wamedai kuwa wamevunjwa moyo wa kuchangia nguvu kazi
zao kwani zinapotea bure.
Walizitaja changamoto zilizopo kwenye vijiji hivyo kuwa ni
tatizo la mawasiliano ambapo wengi wao utembea umbali mrefu kutafuta network
ikiwemo ya kupanda juu ya miti ili simu ziweze kukamata,ukosefu wa barabara
ambapo wamekuwa wakitumia usafiri wa mitumbwi na maboti kufuata huduma za
kijamii kwenye soko,ukosefu wa wauguzi katika kituo cha afya waliopo wapo 3
wanaohudumia watu zaidi ya 6,000 ukosefu wa shule za kata ambapo katika 3 za
mwambao huo hutegemea shule sekondari ya Makonde.
Katika hatua nyingine wananchi wa kata hiyo wameitaka
serikali ya kata hiyo kuwaondoa wananchi wa kitongoji cha Mpasya waliojenga
maeneo hatarishi ambao makazi yao yamezungukwa na visiwa kuwa iwapo hawatahama
maeneo hayo maisha yao yapo hatarini pindi mvua za masika zitakapoanza kunyesha
mfurulizo.
Frank Mapunda mkazi wa kitongoji hico alisema kuwa eneo hilo
lipo bondeni na pia limezungukwa na visiwa vinavyotiririsha maji kutoka katika
milima mirefu iliyopo nyuma ya nyumba hizo hivyo kama hawata tafuta maeneo
mengine ya kujenga makazi mapya basi maisha yao yapo hatarini iwapo mvua za
masika zitaendelea kunyesha.
Alisema serikali ya kijiji hicho pamaja na kata kwa ujumla
iwapo hawatawahimiza wananchi hao kuyahama makazi hayo ambao wameonekana kuwa
wazito kuyahama makazi hayo kwa madai kuwa hawana uwezo wa kujenga nyumba
zingine ambapo baadhi yao walipohojiwa na gazeti hili walidai watahama pindi
watakapo pata pesa.
Alipotafutwa Diwani wa yata hiyo ya Makonde Chrispin
Mwakasungura ofisini kwake lakini hakupatikana na alipopigiwa simu ii kuyatolea
ufafanuzi madai haya simu yake haikupatikana kutokana na tatizo la mtandao wa
mawasiliano linalovikabili vijiji vya
Tarafa hiyo ya Mwambao vilivyopo pembezoni mwa ziwa nyasa.
Na, Ibrahim Yassin
Post a Comment
Post a Comment