IMEELEZWA kuwa kutokana na
kukithiri kwa vitendo vya kishirikina kwenye kitongoji cha Seko Kijiji cha
Njisi kata ya Katumbasongwe Wilayani Kyela mkoani Mbeya wananchi wa kitongoji
hicho wameuomba uongozi wa Serikali ya Kijiji kuwapa kibali cha kumwita Mganga
wa jadi (SANGOMA) kuja kuwasaka wanaofanya vitendo hivyo vya kishirikina
nyakati za usiku.
Wakizungumza na waandishi wa habari jana kijijini humo kwa nyakati tofauti wananchi hao walidai kuwa
kitongoji chao kimeingia doa baada ya kufanyiwa vitendo vya kishirikina nyakati
za usiku kama kufanya tendo la ndoa,upotevu wa pesa kitatanishi,vishindo
kusikika juu ya bati usiku wa manane na milango kugongwa na pindi wanapotoka
nje hawaoni kitu.
Walisema kuwa mbali na
kufanyiwa vitendo hivyo pia wamekuwa wakifanyishwa kazi mashambani nyakati za
usiku bila ya wao kujua na wanapo amka hasubuhi hujikuta wamechoka mwili mzima
hali ya kuwa walilala katika nyumba zao.
Kufuatia vitendo hivyo
wananchi hao waliamua kuitisha mkutano wa hadhara na kuwaomba viongozi wa
kitongoji na kijiji wawape ridhaa ya kwenda kumwita mganga wa jadi(SANGOMA)
nchi jirani ya Malawi ili
alipatie ufumbizi suala hilo.
Walisema uongozi wa kijiji
walisikia kilio chao na kuamua kuwapa ruhusa ya kumwita mganga huyo na kufanya
zoezi hilo kwa amani bila kuvunja amani na utulivu uliopo ambapo siku
iliyofuata mganga huyo alifika na kuanza kazi ya kukagua nyumba hadi nyumba na
kuwabaini watu saba ambao nao walikiri na kuomba msamaha.
Akizungumzia suala hilo
mwenyekiti wa Kitongoji cha Seko Gorden Mwaikeneke aliliambia gazeti hili kuwa
wananchi waliamua kufanya hivyo baada ya kutendewa vitendo hivyo kwa muda mrefu
na mganga alipofika aliwabaini watu saba ambao walitolewa vipembe,hirizi,shanga
na vibuyu vilivyokuwa na vitambaa vyeusi vilivyozungushiwa shanga.
Alisema watu hao waliobainika
walitozwa faini ya laki 3 kila mmoja lakini katika utetezi wao mganga
aliwapunguzia ambapo watu wawili walitao Tsh,200,000 kila mmoja na watu wanne
walitoa Tsh,100,000 kila mmoja na mmoja alitoroka huku idadi iliyokusanywa
ilifikia Tsh,800.000 ambazo aliondoka nazo mganga kama ujira wake kutokana na
kazi aliyoifanya.
Alisema kuwa kufuatia hali
hiyo wananchi walikubaliana kuwa iwapo watu hao wataendelea kufanya vitendo
hivyo basi watafungasha virago na kukihama kitongoji hicho kwani hawatakuwa
tayari kuishi na watu kama hao wanaofanya
vitend vya kishetani.
Afisa mtendaji wa Kijiji cha
Njisi Filimoni Mwafyungulu kwa upande wake alisema kuwa wananchi walifanya
hivyo kama walivyokubaliana wao kama viongozi hawakuhusika kwa kuwa Serikali ya
Tanzania haiamini uchawi hivyo walichokifanya wao ni kusimamia na kuhakikisha
uvunjifu wa amani usitokee na ndivyo hali ilivyo kuwa zoezi lilifanyika kwa
utulivu.
Na, Ibrahim Yassin
Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment