GuidePedia

0
Huyu ni mwenyekiti wa kijiji cha Lusanje NasobileMwandembo.
Huyu ni mwenyekiti wa kitongoji cha Ipomo Omry Mwakomo akijaribu kukwepakwepa madimbwi pamoja na tope katika barabara hiyo
Hawa ni baadhi ya wananchi wakitembea kwa shida katika barabara hiyo.
Huyu nae ni mmoja kati ya wakazi wa kijiji hicho.

                                                           Picha na Lumemo  blog




Wananchi wa kijiji cha Lusanje kata ya mpombo halmashauri ya Busokelo wamemlalamikia mkandarasi wa anaejenga barabara inayotoka kilambo mpaka Nailobi kwakutokamilisha ujenzi wa barabara hio kwa muda muafaka.

Wakiongea na lumemo blog, wananchi hao wasema tatizo la barabara hiyo limekuwa sugu kiasi cha kupelekea kutokuwa na imani na viongozi  wao, kwani nitatizo  ambalo lina zaidi ya miaka miwili sasa.

Aidha wasema kuwa kwa mara ya mwisho mkandarasi alimwaga vifusi pasipokuvisambaza hali inyopelekea barabara hiyo baadhi ya maeneo kutopitika na kulazika kupita porini.

Kwaupande wape mwenyekiti wa kitongoji cha ipomo Omary Mwakomo alisema tatizo hilo limedumu kwa muda mrefa sasa, na kwamba limekuwa kero kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.

Mwakomo amesema tatizo lililopo nikwamba hakuna taarifa maususi kutoka kwa mkandasi anaejenga barabara hiyo kuhusu hitimisho lake.

Hata hivyo mwenyekiti wa kijiji cha Lusanje Nasobile Mwandembo amekiri kuwepo kwa tatizo hilo na kesema moja kati ya sabaabu ya kucheleweshwa kwa ujenzi huo ni kutokana na mkanganyiko uliokuwepo kati ya kandarasi na kamati ya ujenzi ya kijiji hicho.

Mwandembo amesema mkanganyiko huo ulitokea baada ya mkandarasi kudai gharama za ujenzi huo  ni shilingi milioni kumi na tano, huku kamati ikidai shilingi milioni kumi.

Mwandembo amesema kutokana na mkanganyiko huo ndio uliosababisha kulegalega kwa ujenzi na mpaka sasa barabara hiyo inatengenezwa kwa gharama ya shilingi milioni kumi.

Post a Comment

 
Top