WATU
WATATU WAFARIKI DUNIA BAADA YA GARI WALILOKUWA WAKISAFIRIA KUACHA NJIA
NA KUPINDUKA HUKO KATIKA KIJIJI CHA MWAMBEGELE KATA YA KYIMO, TARAFA YA
UKUKWE BARABARA YA TUKUYU/MBEYA WILAYA YA RUNGWE. AJALI HIYO ILITOKEA
MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 16:00HRS JIONI BAADA YA GARI
LENYE NAMBA ZA USAJILI T.873 BZA/T.501 CCZ AINA YA HOWO TRUCK MALI
YA CHAINER TRUCK COMPANY LTD LILILOKUWA LIKIENDESHWA NA DEREVA JOHN
MATHIAS @ MWIMBILIZYE (40), MKAZI WA DSM, LIKIWA LIMEBEBA MAKAA YA MAWE
KUTOKA NCHINI MALAWI KUELEKEA DSM KUACHA NJIA NA KUPINDUKA KISHA
KUSABABISHA VIFO VYA WATU WATATU AMBAO NI DEREVA WA GARI HILO, PAMOJA NA
WATU WENGINE WAWILI WALIOFAHAMIKA KWA JINA MOJA MOJA ISAYA, MIAKA KATI
YA 43-45, DALALI, MKAZI WA UYOLE NA SALUM, MIAKA KATI YA 40-42,
MSAIDIZI WA DEREVA. PIA MAJERUHI NI HAMISI RAMADHAN (40), DALALI, MKAZI
WA UYOLE. CHANZO CHA AJALI KINACHUNGUZWA. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA
HOSPITALI YA MAKANDANA TUKUYU NA MAJERUHI AMELAZWA HOSPITALINI HAPO.
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI
ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA MAKINI WANAPOTUMIA VYOMBO
VYA MOTO KWA KUFUATA/KUZINGATIA SHERIA NA ALAMA ZA USALAMA BARABARANI
ILI KUEPUKA AJALI ZINAZOWEZA KUEPUKIKA.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI.
JESHI
LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA
LA SPRIANO WILSON (40), MKAZI WA IFUMA AKIWA ANAMILIKI SHAMBA LA BHANGI
LENYE UKUBWA WA ROBO HEKTA LIKIWA NA MICHE YENYE UREFU WA FUTI TATU
[03]. MTUHUMIWA ALIKAMATWA KATIKA MSAKO ULIOFANYIKA MNAMO TAREHE
25.02.2014 MAJIRA YA SAA 11:30HRS ASUBUHI
HUKO
KATIKA KITONGOJI CHA KAGERA, KIJIJI CHA IFUMA, KATA YA LUPA, TARAFA
YA KIPEMBAWE WILAYA YA CHUNYA. MTUHUMIWA NI MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI
WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA
WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI WA POLISI ROBERT MAYALA
ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA
YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA
JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI
YAO.
JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LINAMSHIKILIA MTU MMOJA AKIWA NA MICHE 27 YA BHANGI KATIKA SHAMBA LAKE.
MTU
MMOJA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA ISRAEL MWAMBENE (39), MKAZI WA SIMIKE
ANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA AKIWA NA MICHE YA BHANGI
27, YENYE UREFU WA FUTI 2.5 ALIYOKUWA AMELIMA KWENYE SHAMBA LA MIGOMBA.
MTUHUMIWA ALIKAMATWA MNAMO TAREHE 25.02.2014 MAJIRA YA SAA 12:20HRS
MCHANA HUKO KATIKA KITONGOJI CHA MALIBILA, KIJIJI CHA SIMIKE, KATA YA
LUFINGO, TARAFA YA UKUKWE WILAYA YA RUNGWE. MTUHUMIWA NI
MKULIMA/MUUZAJI NA MTUMIAJI WA BHANGI. TARATIBU ZA KUMFIKISHA MAHAKAMANI
ZINAFANYIKA. KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA KAMISHINA MSAIDIZI
WA POLISI ROBERT MAYALA ANATOA WITO KWA YEYOTE MWENYE TAARIFA ZA
MTU/WATU WANAOMILIKI MASHAMBA YA BHANGI NA WANAJIHUSISHA NA
UUZAJI/USAMBAZAJI WA BHANGI AZITOE KWA JESHI LA POLISI ILI WAKAMATWE NA
HATUA ZA KISHERIA ZICHUKULIWE DHIDI YAO.
Signed by:
[ROBERT MAYALA – ACP]
KAIMU KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA.
Post a Comment
Post a Comment