Mgeni rasmi Adeny Mwakyonde aliyevaa suti ya kijivu pamoja na mpambe wake alipokuwa akiingia uwanjanjani
MC E, Mwinuka alipokuwa akifanya ushereheshwaji wakati wakumpokea mgeni rasmi
Mgeni rasmi alipokuwa anaenlekea kukaa katika meza kuu pamoja na wapambe wake.
MC E, Mwinuka alipokuwa akifanya ushereheshwaji wakati wakumpokea mgeni rasmi
Mgeni rasmi alipokuwa anaenlekea kukaa katika meza kuu pamoja na wapambe wake.
Kundi la Comedy lilipokuwa litumbuiza katika uzinduzi wao. Hii ndio CD iliyozinduliwa |
Kiongozi wa kundi la Comedy Lusekelo Mwang'amba akisoma lisala kwa mgeni rasmi.
Mgeni Rasmi alipokuwa akijibu risala kutoka kwa msomaji
Mgeni rasmi alipokuwa akiondoka katika viwanja vya sherehePicha na Lumemo blog ...................................................................................................................................................................................
Vijana wametakiwa kujituma katika kufanya kazi za zakujiajiri na kujipatia
kipato ili kuondokana na wimbi la umasikini linalowakabili vijana.
Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya siasa ya chama cha
Mapinduzi CCM mkoa wa mbeya Adeny Mwakyonde alipokuwa katika uzinduzi wa filam
ya vichekesho (COMEDY)uliyofanyika jana katika kijiji cha Lusanje kata ya
mpombo halmashauri ya Busokelo iliyochezwa na kundi la msukuma Comedy.
Mwakyonde ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa chama cha
Mapinduzi (CCM) Taifa amesema kuwa moja kati ya ajira sahii na yauhalali ni kucheza filam kwani vijana wengi wa mijini kwa sasa wamejikita katika
kuelimisha jamii kwa njia ya maigizo.
Mwakyonde ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa
filam hiyo iliyojulikana kwa jina la msukuma Comedy, alilipongeza kundi hilo
kwakujituma kufanya kazi yenye tija katika jamii.
Aidha Mwakyonde aliliunga mkono kundi hilo kiasi cha shilingi
laki nne keshi na kuahidi kuwaongezea shilingi laki moja na kuwatafutia
wadhamini sehemu mbali mbali ili kuwaendeleza vijana hao.
Nae mgeni aliyeongozana na mgeni rasmi Furaha Mwambungu
amesema nijitihada nzuri walizozifaya vijana hao hivyo hana budi kuwaponmgeza
kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii, pia amewaunga mkono kwa kiasi cha shilingi
elfu hamsini na kuahidi kuwaongezea shilingi elfu hamsini nyingine siku za hivi
karibuni.
Hata hivyo kiongozi wa kundi hilo Lusekelo Mwakang’amba amesema anawashukuru
watu wote waliyoitikia wito huo kwakujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono kwa
hali na mali.
Aidha amemshukuru mgeni rasmi kwakuacha kazi zake kuja
kuhudhuria uzinduzi huo na kuwaunga mkono kiasi cha shilingi laki nne keshi
pamoja na mgeni aliyeongozana nae kwakuwaunga mkono kiasi cha shilingi elfu
hamsini keshi.
|
Post a Comment
Post a Comment