Mwenyekiti wa wenyeviti Antony Mwalugembe akitoa mrejesho
.............................................................................................
WENYEVITI wa
Serikali za vijiji katika jimbo la Rungwe Magharibi Wilayani Rungwe mkoani
Mbeya wamegoma rasmi kufanya kazi za
Serikali katika vijiji vyao kutokana na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya
hiyo kushindwa kuwapa stahiki zao.
Tamko hili
limefanyika leo katika mkutano mkuu ulioitishwa na wenyeviti wote wa jimbo hilo
uliofanya kwenye viwanja vya shule ya msingi Bulyaga kata ya Kawetele mjini
Tukuyu na kuhudhuriwa na mamia ya wakazi
wa wilaya hiyo walioonekana kuwaunga mkono wenyeviti hao.
Akizungumza katika
mkutano huo Mwenyekiti wa wenyeviti
wilayani humo Anton Mwalugembe alisema kuwa siku ya tarehe 12 mwezi huu yeye
pamoja na viongozi wenzake waliitwa na mkuu wa wilaya Chrispin Meela ofisini
kwake kwa ajili ya kulizungumzia suala hilo huku akiwashirikisha Mkurugenzi wa
halamashauri hiyo Gwabo Mwansasu,mwenyekiti wa halmashauri Mwakipiki
Mwakasangula pamoja na katibu tawala na afisa utumishi.
Mwalugembe alidai
kuwa mkuu wa wilaya alitaka kujua tatizo lao ambapo alimueleza kuwa wao wanataka
kulipwa posho zao kwani tangu waingie madarakani miaka kumi iliyopita
hawajawahi kulipwa posho kama ilivyo
agizwa bungeni, tarehe 31 agosti 2013,wala semina pamoja na serikali
kutothamini mchango wao katika shughuri za maendeleo.
Alisema baada ya maelezo hayo mkuu huyo wa
wilaya aliiagiza halmashauri kusikiliza na kuyatekeleza madai ya wenyeviti kwa
kuanza kuwapa semina kabla ya ushaguzi ujao na kuwataka wenyeviti kusuburi
kwani suala la posho pamoja na kuwa bunge lilitangaza lakini halijaanza
kutekelezwa.
Alieleza kuwa
leo tarehe 14 februari 2014 alitoa mrejesho wa yale yote waliyoelezwa na mkuu
wa wilaya ili wajumbe wachangie katika kuchangia wenyeviti hao walipinga hatua hiyo na kudai kuwa hizo ni
siasa hakuna kitakachofanyika.
Steven
Mwakasenge mwenyekiti wa kijiji cha Iringa kata ya Ibigi alisema kuwa yeye
amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 na anapitwa bila kupingwa kupitia CCM lakini
serikali ya chama hicho imekuwa haiwajali wenyeviti wakati ndiyo wanaofanikisha
shughuri zote za maendeleo katika wilaya hiyo na kuwa kuanzia leo wanasaini
kufanya mgomo wa kusimama kufanya kazi katika vijiji vyao hadi pale watakapo
pewa stahiki zao.
“haiwezekani
sisi tufanye kazi katika mazingira magumu huku shughuri za maendeleo sikisonga
mbele alafu posho wapewe maafisa watendaji pamoja na madiwani wakati wao ndiyo
chachu ya maendeleo alafu wasipewe posho haiwezekani ni lazima tugome”alisema
Mwakasege.
Kutokana na
kauli hiyo wenyeviti wote bila kinyongo kwa hiyari yao waliandika majina yao na
kuweka sahihi ya kukubari kuweka mgomo wa kutofanya kazi tena hadi pale
watakapopewa stahiki zao zote maamuzi ambayo yaliungwa mkono na mamia ya
wananchi walihudhuria mkutano huo.
Wananchi kwa
upande wao waliwapongeza wenyeviti hao kwa ujasiri waliouonyesha wa kufanya
maamuzi magumu ya kuendesha mgomo na kusema kuwa ipo haja ya Serikali wilayani
humo kuliangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo kwani linaweza likaharibu mfumo
mzima wa utawala bora kwa kuwa wenyeviti ndiyo wenye watu.
Kaimu
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Gwabo Mwansasu alipofuatwa na
waandishi wa habari ili kulizungumzia tatizo hilo hakuweza kuzungumza chochote.
Post a Comment
Post a Comment