Mwenyekiti aliyesimamishwa
uongozi ni Mchungaji Nosigwe Buya ambapo baadhi ya Watumishi, Waumini na
Wachungaji wa Kanisa hilo kupinga maamuzi ya kuondolewa kwa Mwenyekiti kwa
madai kuwa maamuzi hayo yalikiuka katiba ya katika.
Kutokana na kuwepo kwa
mtafaruku ndani ya kanisa hilo, Baadhi ya Wachungaji wapatao 25 wa kanisa hilo
walijitokeza mbele ya vyombo vya habari wakitoa tamko kali la kuutaka
kurejeshewa kwa madaraka yake Mwenyekiti huyo ili kunusuru kuvunjika kwa
kanisa.
Wachungaji hao ambao
walimchagua Mchungaji Chilale Edward Simoni kuwa Mwenyekiti wao na Daudi
Mwiligumo kusoma tamko waliloliandaa linalopinga maamuzi ya kusimamishwa
uongozi Mwenyekiti wao wa Jimbo na kuitaka Mahakama kuingilia kati.
Akisoma tamko hilo, Mchungaji
Mwiligumo alisema jambo wanalopingana nalo ni
pamoja na kikao cha kumsimamisha Mwenyekiti kilivunja katiba ya kanisa
iliyosahihishwa na kusanifiwa mwaka 2012 ibara ya 11 kifungu cha 4(iv).
Alisema kifungu hicho kinasema
Mwenyekiti asipokuwepo, Makamu mwenyekiti atakuwa mbadala yake na ibara ya 35
inasema wakati wowote Mwenyekiti asipokuwepo Makamu atakuwa Mwenyekiti lakini
katika kikao kilichomuondoa Mwenyekiti wao hata Makamu hakuwepo hivyo kikao
kilikosa uongozi.
Aliongeza kuwa katika kikao
kilichofanyika Julai 31, Mwaka jana kilimuondoa Katibu Mkuu ambaye kwa mujibu
wa Katiba ibara ya 36(2)(ii) ambacho kinataja moja ya kazi za katibu ni
kuandika Muhtasari wa kikao hivyo kikao
hicho hakikua halali kutokana na watendaji wakuu kutokuwepo.
Tamko hilo liliendelea kudai
katiba ya kanisa hilo iliendelea kuvunjwa baada ya Muumini wa kawaida
aliyetajwa kwa jina la Charles Mwakipesile kukalia kiti kinyume cha ibara ya
10(2)C ambacho kinasema Mwenyekiti na makamu sharti wawe wachungaji.
Walisema kwa mujibu wa katiba
mwenyejukumu la kumuondoa kiongozi yeyote katika nafasi yake ni Mkutano mkuu wa
Sinodi unaohusisha wajumbe wengi na kwamba Mwenyekiti aliyeondolewa
alichaguliwa kihalali na Sinodi mwaka 2012.
Mbali na hilo wachungaji hao
walidai vipengere vingine kukiukwa ni pamoja na kumdalisha kazi Mwenyekiti huyo
kinyume na utaratibu ikiwa ni pamoja na kumpangia katika kituo kipya cha kazi
ambayo ni ya chini kuliko wadhifa aliyokuwa nao.
Pia walipinga kitendo cha
Kutakiwa Mwenyekiti huyo kuhama katika nyumba za kanisa hadi kufikia Februari
7, Mwaka huu kinyume cha utaratibu uliwekwa na kanisa hiloambao kila kiongozi
wa Kamati tendaji hutakiwa kuishi katika nyumba zilizo ndani ya Makao makuu ya
Jimbo.
Waliongeza kuwa juhudi zao zote
ni kutaka kulinusuru kanisa na kuiomba Mahakama na vyombo vya Dola kuingilia
kati kwa kumtambua Mwenyekiti wa Jimbo Mchungaji Buya kuwa ndiye Mwenyekiti
halali wa Jimbo na kuiamuru Halmashauri ya jimbo na kamati tendaji pamoja na
Askofu Alinikisa Cheyo kuitisha Mkutano wa Sinodi haraka kwa ajili ya maamuzi.
Aidha mgogoro unaoendelea ndani
ya kanisa hilo pia umemhusisha moja kwa moja Askofu wa jimbo hilo, Alinikisa
Cheya na kwamba kuna watu wachache wanataka kulitumia kanisa kama taasisi
binafsi kujinufaisha wao wenyewe.
(Na, Ezekiel Kamanga)
Post a Comment
Post a Comment