Mgeni rasmi Aden Mwakyonde Mwambepo alipokuwa anawasili katika viwanja vya sherehe
Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiria mali State Mwaipasi akisoma risala kwa mgeni rasmi
Mgeni rasmi akiwa katika msafara wa kukagua vyumba vya biashara.
Baadhi vyumba vya biashara katika eneo hilo
Mwenyekiti wa kijiji cha mbigili Gwakisa Mwamlenga alipokuwa akimshukuru mgeni rasmi.
Mgeni rasmi alipokuwa akienda mbele kujibu lisala ya wajasiriamali.
Burudani za ngoma aina ya mang"oma zikiendelea katika viwanja vya sherehe
Mgeni rasmi akipewa zawadi ya mbuzi na mkungu wa ndizi na wazee wa kijiji hicho.
Mgeni rasmi alipokuwa amekaa katika kiti chake jukwaa kuu alivaa suti nyeusi hapo mbele
Hii ndiyo lisala ya kikundi kwa mgeni rasmi.
Wajasiriamali wa kijiji cha mbiligili kata ya Lwangwa
Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya wamepongezwa kwa juhudi zao walizozionesha
katika kujenga vyumba vya maduka kwaajili ya kupangisha kama mradi wa kikundi
hicho.
Pongezi hizo zilitolewa na Mjumbe wa kamati ya siasa ya chama
cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mbeya na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Bw,
Aden Joseph Mwakyonde Mwambepo alipoalikwa katika hafla ya uzinduzi wa vyumba
hivyo uliyofanyika jana katika kijiji cha mbigili kata ya lwangwa Halmashauri
ya Busokelo.
Aden Mwambepo amesema kumekuwa na vukundi vingi vya
wajasiriamali vikianzishwa sehemu mbali mbali lakini mafanikio yake ni machache
tofauti na kikundi kilichopo katika kijiji hicho, hivyo ana kila sababu ya
kuwapongeza wanakikundi kwajuhudi zao walizozifanya katika kubuni mradi huo.
Aden Mwambepo ambae pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi huo amewataka wanakikundi
wengine ambao hawana biashara ya kufanya, wajitahidi kutafuta mitaji kwa njia
halali ili waweze kufanya biashara, “kutokana na jitiada hizo mlizoenesha sina
budi kuwapongeza kwa kazi nzuri na kwa wale wajasiriamali wote ambao hawajaanza
kufanya biashara huu ndio wakati wao wa kufanya biasha kwa maana fursa iliyopo
inatosheleaza kufanya biashara”
Aidha Adeni Mwambepo alimpongeza Prof, Mwakyusa na Mwandosya
kwa kazi nzuri walizozifanya za kupeleka umeme kila sehemu ya halmashauri hiyo,
kwani umeme ndiyo chachu ya maendeleo katika jamii, “ nampongeza sana Prof
Mwakyusa na Mwandosya kwakutuletea umeme maana sasa tunauwezo wakufanya biashara mpaka usiku kwasababu mwanga upo,
jamani wana lwangwa tutumie fursa hiyo katika kuleta maendelo ya Halmashauri
yetu”
Hata hivyo Aden Mwakyonde Mwambepo katika kuwaunga mkono
wajasiriamali hao aliwachangia kiasi cha fedha taslimu shilingi milioni moja
1,000,000/= “nimefurahi sana kwakunipa heshima hii wana mbigili maana hii ni
heshima ya kipekee sana, mngeweza kumpatia mtu mwingine yeyote lakini mkaona
mnipatie mimi, jambo lingine nimefurahi sana kwa juhud zenu za ujenzi wa
vibanda hivyo kwaiyo mimi ninawachangia fedha keshi shilingi milioni moja.
Nae mweyekiti wa kikundi hicho State Mwaipasi kwaniaba ya
wanachama wake amesema anamshukuru sana mgeni rasmi Aden Mwakyonde Mwambepo
kwamchango wake aliyoutoa wa fedha pamoja na kuacha kazi zake kwaajili ya
kuwasikiliza katika hafla yao.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment