GuidePedia

0

Mkuu wa idhaa ya kiswahili ya sauti ya amrica washngton Mwamoyo Hamza akiwa katika viwanja vya kampeni

Muandaaji wa vipindi vya je, nifanyeje? Bi, Lucy Patrick akiwa katika viwanja vya kampeni hiyo



Wanafunzi na wageni waalikwa  wakiangalia kampeni hiyo.


Katika kampeni hiyo vijana walishauriwa na mama ushauri Martha Haule ambae ni mtangazaji wa Highlands fm 


Vijana wa lika mbali mbali mkoani Mbeya wametakiwa kutumia fursa zinazojitokeza katika nyanja mbali mbali na kuwa makini pindi wanapotaka kufanya maamuzi yao.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa mbeya Mh, Abasi Kandoro aliyewakilishwa na mkuu wa wilaya ya mbeya Mh, Norman Sigala katika kampeni iliyoaandaliwa na shirika la utangazaji la idhaa ya Kiswahili ya sauti ya America washngton iliyofanyika katika viwanja vya Ruanda nzovwe jijini Mbeya.
Kandoro amewashkuru waandaaji wa warsha na kwamba kupitia kampeni hiyo vijana wamepata ujuzi wa kutosha hivyo vijana wenyewe wanatakiwa kufanyia kazi yale yote ambae waliyoelekezwa katika warsha hiyo.

Aidha amesema kumekuwa na tabia ya baadhi ya vijana kujiingiza katika mahusiano pasipo kujiuliza hivyo wanatakiwa kabla hawajafanya jambo lakujiingiza katika mahusiano pamoja na mambo mengine ni lazima wakatumia kauli ya kampeni hiyo ya je, nifanyeje?

Kwa upande wake mkuu wa idhaa ya Kiswahili ya sauti ya America washngton Mwamoyo Hamza amesema amefurahishwa na mwitikio mzuri wa vijana na kwamba kupitia kampeni hiyo vijana wengi watanufaika na maelekezo waliyoyapata.

Amesema lengo kuu la kampeni hiyo ni kuwawezesha vijana kufanya maamuzi sahii katika masuala ya afya na masuala ya kijamii na kwamba wanataka kijana kabla hajafanya maamuzi katika suala lolote linalomuhusu ajiulize je, nifanyeje?

Mwamoyo amesema kijana anapopata muda wa kujiuliza kuhusu jambo Fulani anakuwa na umaamuzi sahii ambayo yatamsaidia katika kundesha maisha yake pamoja na afya yake.

Nae muandaaji wa vipindi vya je, nifanyeje mkoa wa mbeya Bi, Lucy Patrick amesema vijana wanatakiwa kupewa kipaumbele katika taifa hili na kutoa ushauri kwa vyombo vya habari vingine kutoa elimu kwa vijana inayohusu afya pamoja na uamuzi sahii.

Hata hivyo Bi, Lucy amesema vijana waliyohudhuria katika kampeni hiyo pamoja na wanafunzi kutoka katika shule za Secondary tano jijini, ikiwemo secondary ya Ivumwe, Meta, Loleza, Sangu na Mbeya day.

                    Na, Lumemo blog




Post a Comment

 
Top