SHIRIKA la
The Struggle For Community Support Alliance (SCSA) yenye makao makuu yake
wilayani Kyela mkoani Mbeya jana limetangaza neema kwa wananchi wa wilaya hiyo
ya kuwaletea mradi wa gesi asilia au gesi hai (BIOGAS) utakao anza mwezi march
mwaka huu.
Akizungumza
jana na waandishi wa habari ofisini kwake mwenyekiti wa shirika hilo kitaifa Dk,Abraham
Mwanyamaki alisema asasi yake imesajiliwa kwa ngazi ya Taifa kwa ajili ya
kufanya kazi za kusaidia jamii upande wa Afya,Elimu,Michezo,Mazingira na ujasilia
mali na kuwa kwa mwaka wa kwamza tayari wamesaidia Sekta ya elimu na michezo.
Alisema kuwa
mwaka huu wa 2014 Shirika lake litajikita kuleta mradi wa Gesi hai kwa kila
kata ambapo wananchi watatakiwa kujiunga katika vikundi kwa ajili ya kuwezeshwa
kupatiwa mradi huo ambao utawapunguzi tatizo la kutembea umbali mrefu kufuata
kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia na badara yake watatumia gesi hai
itakayotengenezwa na wao wenyewe.
Mwanyamaki
aliongeza kuwa Shirika lake kwa kushirikiana na wafadhiri mbalimbali wakawemo
wakala wa umeme vijijini (REA) ambao wamewapatia mitambo yakuanzia kufunga
kwenye kila kata ili wananchi waanze kunufaika na mradi huo ambao utasaidia
kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kuwa taka ngumu ndizo zitakazotumika katika
mradi huo.
Alisema kuwa
anawataka wananchi kuwa tayari kuupokea kwa mikono miwili mradi huo ambao
wataanza kufunga mitambo miwili kwenye kata za Ipande na Kasumulu kwa kufuata
maelekezo kutoka kwenye Halmashauri ya Wilaya Idara ya mifugo ambao ni wadau
wakubwa wa mrad huo.
Aliongeza
kuwa mwezi wa tatu mwaka huu watakapofunga mitambo hiyo kwenye kaya hizo
watatoa mafunzo kwa wananchi watakao jiunga kwenye vikundi namna ya kutumia
mradi huo ili kuleta ufanisi katika matumizi sahihi ili wasipate madhara.
Hata hivyo
Mwenyekiti huyo amewasisitiza wananchi hao kuacha kusikiliza propaganda
zinazoenezwa na baadhi ya wanasiasa wasioitakia mema wilaya hii na kuwa katika
suala la maendeleo siasa ikae pembeni kwani inakwamisha juhudi za kumkwamua
mwananchi katika lindi la umasikini.
Post a Comment
Post a Comment