GuidePedia

0


Katikati ni mwenyekiti wa jumuiya ya wafanyabiashara Tanzania Bw,Johnson Minja kushoto ni mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabishara mkoa wa mbeya  Bw, Charles Syonga.



Baadhi ya waandishi wa habari mkoa wa mbeya wakiwa katika kikao hicho na viongozi hao wa kiaifa wa jumuiya hiyo.



Jumuiya ya wafanyabishara Tanzania imetolea ufafanuzi juu ya tatizo la kulalamikia mashine ya kutolea risiti ya kielektroniki (EFDs) sababu kuu inayowafanya wafanyabiashara waikatae mashine hiyo.

akiongea na waandishi wa habari katika ofisi ya wafanyabiashara iliyoko maeneo ya magorofani jijini Mbeya mwenyekiti wa Jumuiya hiyo Taifa Bw, Johnson Minja amesema amesema kuwa sababu inayowafanya kugomea mashine hiyo namna inavyofanyakazi isivyo sahii.

Aidha amesema mashine hiyo imekuwa ikiangalia upande mmoja tu ambao ni upande wa mauzo tu badala ya kuangalia gharama za manunuzi, gharama za uendeshaji na kisha iangalie faida na baada ya hapo ndipo ikate kodi katika faida badala ya kukata kwenye mauzo.

Minja amesema wafanyabiashara hawaikatai mashine hiyo bali wanakataa mfumo wake uanavyofanyakai kwani kunauwezekao wa kubadili mfumo huo na pindi serikali watakapo madirisha mfumo huo wao hawana sababu ya kugomea mashine hizo kwa zitakuwa hazina madhara yeyote kwa mfanyabiashara.

Akitolea mfano namna mfanyakazi anavyokatwa kodi yake Manji amesema mfanayakazi anakatwa kodi kwenye kipato chake na si mtaji kwaana hiyo angekuwa anakatwa kwenye mtaji basi angeweza kukatwa akiliyaani uwezo wa kufanayakazi.

Vivyo hivyo mfanyabiashara anakatwa akili yaani ule mtaji wake maana mashine hiyo inaangalia mauzo tu kwani mauzo hayo ukipiga hesabu kama umeuza bidhaa ya shilingi ekfu kumi basi uwenda faida yake ikawa shilingi mia tano hivyo mashine hiyo inakata kulingana na mauzo yale uliouza ya shilingi elfu kumi kwaiyo itakuwa imekata mpaka mtaji.

hata hivyo Minja amesisitiza wafanyabiashara kuhudhuria katika mkutano unaotarajia kufanyika siku ya juma nne ya tarehe 9 mwezi wa kumi na mbili katika ukumbi wa mtenda uliopo soweto ili kuzungumza mambo yanayowahusu wafanyabiasha hayo wa jiji la mbeya, ambapo katika mkutano huo kutakuwa na viongozi mbali mbali wa kitaifa katika jumuiya hiyo kutoka makao makuu jijini Dar es salaam.

                            Na, Lumemo blog

Post a Comment

 
Top