Mkazi mmoja wa kijiji
cha mwela wilayani rungwe mkoani mbeya Sela
mwakasendele mbogoso miaka {33} ameingia
kwenye wakati mgumu baada ya kunyofolea
kwa kung’atwa sikio na jicho lake la
kushoto na mumewe fati mwasumbwe kutokana na
kile kilicho daiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Hayo
yamejili usiku wa kuamkia janual {1}
mwaka huu ambapo bila kujua hili wala lile
mama huyo alijikuta akiingia kwenye wakati mgumu
baada ya kurejea nyumbani kwake majira ya
usiku wa manane huku akiwa amelewa
pombe kufuatia kileo hicho kimepelekea
kutofautiana na mumewe hivyo kuanza kushambuliwa na mume ikiwa
ni pamoja na kunyofolewa kwa kung’atwa
sikio na jicho la kushoto na kupelekea
kupoteza damu nyingi zaidi.
Mashuhuda wa waliokuwepo eneo la tukio wamesema
tukio hilo limetokea baada ya mama huyo kuchelewa
kurejea nyumbani kwake ndipo kutokana na hali hiyo
mume alijikuta amejawa na hasira
na kuanza kumuadhibu vikali mkewe.
Aidha alisema watu hao
kugombana imekuwa kawaida yao na kwamba
kila ifikapo nyakati ya usiku huwa wanawasumbua
kwa kuwapigisha kelele na kuamua
kufikia hatua ya kuwakamata kwa kuwa
fikisha kwenye kwenye vyombo vya sheria ili kutatua tatizo
lao.
Kwa upande wa mama huyo alisema
chanzo ni baada ya mumewe kumuhisi
kwamba mkewe ana wanaume
wengine na kwamba yeye huwa
anachelewa virabuni kuuza pombe .
Kwa upande wake mume na
mwanamke huyo amesema amefikia hatua hiyo baada
ya kuchoka na tabia za mkewe kwani kila siku amekuwa
mtu wa kurumbana naye na kwamba ili kupunguza
kiburi chake akamua kumuweka alama ya kutosha ili
iwe fundisho na kwa wengine.
Mtendaji wa kijiji hicho
Neema Ipopo licha ya kukiri
kutokea kwa tukio hilo amesema mpaka sasa Serikali imewapatia
kibari cha kwenda hospital kwaajili ya
kutibiwa huku hatua
zingine za kisheria zikichukuliwa dhidi yao.
Na, Baraka Lusajo rungwe
Post a Comment
Post a Comment