Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa mbeya, Allan Mwaigaga akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti huyo wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa mbeya.
Mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani mkoa wa
mbeya Allan Mwaigaga amewataka madereva kuwa makini pindi wawapo barabarani kwa
lengo la kuepuka ajali zisizokuwa za lazima.
Kauli hiyo ameitoa jana alipokuwa akiongea na
waandishi wa habari ofisini kwake kufuatia ajali zilizotokea mfululizo hivi
karibuni ikiwemo ajali ya basi la abiria iliotokea juzi mlima nyoka jijini
mbeya.
Mwaigaga amesema asilimia kubwa ya ajali zinazotokea
zinasababishwa na makosa ya kibinadamu ambayo yanaweza kuepukika ili hali
madereva wakiwa makini na kuzingatia sheria za barabarani.
Aidha Mwenyekiti huyo amesema kumekuwa na imani potofu
ya baadhi ya watu kuhisi kuwa wamiliki ndio wanaosababisha ajali kwa madai ya
kutoa kafara jambo hilo si la kweli.
“kuna baadhi ya watu wanadhani kuwa kuna
uhusiano kati ya ajali zinazotokea na wamiliki pamoja na kuhisi kuwa inapofika
mwisho wa mwaka ndio ajali nyingi hutokea jambo hilo sio la kweli hata kidogo
bali ni uzembe wa madereva na kuhusu
kuongezeka kwa ajali mwisho wa mwaka
ikumbukwe kuwa mwisho wa mwaka kunaambatana na sikuku hiyo madereva
wengi wanatumia nafasi hiyo kuendesa huku wakiwa wamelewa, hivyo nawaasa
madereva waache tabia ya ulevi pindi wawapo barabarani” alisema Mwaigaga.
Mwaigaga aliongeza kuwa licha ya kuelekea kipindi cha sikuku pia kipindi hiki mvua ndio
zimeanza hivyo barabara zinakuwa sio nzuri kutokana na mvua kunyesha mara kwa
mara.
Na kuhusu ongezeko la ajali Mwenyekiti huyo amesema
takwimu za kitaifa zinaonesha ajali zimepungua japo si kwa kiwango kikubwa lakini
anaamini elimu wanayoendelea kuto kwa madereva na abiria ajali itazidi kupungua
zaidi kwa kumekuwa na ukosefu wa elimu ya usalanma barabarani.
Pia amewataka wamiliki wa vyuo vya udereva nchini
kuelekeza sana elimu ya usalama barabarani kwa wanaojifunza masuala ya udereva.
Hata hivyo Mwaigaga amesema matatyizo mengine
yanachangiwa na wamiliki wa vyombo vya moto bandia ambao hawatakikujitokeza
katika vyama vya wamiliki wa vyombo vya moto ili kupeana elimu juu ya umiliki
na jinsi ya kuwabana madereva ambao si waadilifu, hivyo ametoa wito kwa
wamiliki wote ambao hawajajiunga katika vyama vya wamiliki wa vyombo vya moto
wajitokeze ili kushirikiana kwa pamoja na kuwabana madereva hao ambao
wanasababisha ajali zisizo za lazima.
Na, Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment