Afisa wa kilimo wilaya ya Mbinga Bw, Yonasi Nyoni alipokuwa akiongea na mwandishi wa Mtandao huu Ofisini kwake.
Baadhi ya wakulima waliyoathirika na pembejeo hizo ambao wengine ni viongozi wa serikali ya mtaa katika wilaya hiyo walipokuwa wakiongea na mwandishi wa Mtansdao huu.
Afisa ukaguzi wa pembejeo kutoka katika ofisi ya kilimo wilaya ya Mbinga Bw, Andrew Chiwinga.
BAADHI ya wakulima
wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wameiomba serikali kutowaonea aibu
wafanyabiashara wa Pembejeo wenye tamaa
ya kujipatia faida kubwa kwa kuuza bidhaa feki, hivyo kuhatarisha usalama wa
chakula na kuwapunguzia mavuno.
Hayo yalisemwa jana na wakulima hao walipohojiwa na Mtandao
huu wamesema,serikali inapaswa kusimamia usambazaji wa pembejeo kote nchini ili
kudhibiti uingizwaji wa bidhaa feki ambao umeanza kushamiri katika kipindi cha
hivi karibuni.
John Kapinga mkulima katika kitongoji cha Lusaka alisema kitendo cha kuuziwa pembejeo feki wakulima, kinawarudisha
nyuma na kuwafanya washindwe kutimiza malengo yao ya kiuchumi ikiwa ni pamoja
na kukabiliana na harakati za kuondoa
umasikini.
“katika msimu uliopita
nilinunua mbolea aina ya chumvi chumvi (SA), lakini nilipoiweka shambani
haikuonesha matokeo mazuri, hali ambayo ilinifanya nisipate mavuno mazuri ikilinganisha nay a misimu mingine” alisema
Kapinga.
Kapinga alisema serikali isiwaachie wafanyabiashara wafanye
watakavyo na kwamba wakiachiwa wanaweza
kuliangamiza taifa kwa kulikosesha chakula na kudidimiza uchumi wa wakulima.
Akizungumzia suala hilo Ofisa Kilimo wilayani Mbinga Yonasi
Nyoni alisema tatizo hilo limejitokeza katika kijiji cha Liula ambapo ofisi
yake ilichukua hatua ya kwenda kukagua ambapo hali ya mazao shambani walikuta
ni mbaya ukilinganisha na matarajio baada ya kuweka mbolea hiyo na ndipo
walipochukua sampuli ili kuzifanyia utafiti.
Amesema mbolea hiyo aina ya Chumvichumvi ilipopimwa ilikutwa
ina kiwango kidogo cha Nitrojen cha asilimia mbili badala ya 21, kiwango
ambacho hakiwezi kuleta tija shambani, hali hiyo ilifanya muuzaji kuchukuliwa
hatua kwa kufunguliwa mashitaka katika mahakama ya mwanzo Mbinga na kesi No.
43/2014.
Amewataja washitakiwa katika kesi hiyo kuwa ni Hamisi Nakanga
na Dastan Kombe ambao walikuwa wakiwakopesha wakulima mbolea hizo kwa
makubaliano ya wakulima kulipa mahindi gunia mbili na robo za mahindi baada ya
mavuno ya msimu unaokuja.
Nyoni alisema serikali
wilayani hapa imeweka mkakati wa kukagua pembejeo katika maduka kila baada ya
miezi mitatu ikiwa ni pamoja na kuwasajili mawakala wauzaji pembejeo na
kuwahamasisha wakulima kununua pembejeo kwa mawaka waliosajiliwa na wadai
stakabadhi kila wanunuapo bidhaa hizo.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Mbinga
Oska Yapesa alikiri kupokea malalamiko ya wananchi kuhusiana na kuuziwa mbolea
feki na kwamba hata yeye aliwahi kuuziwa
Mbegu feki huko Dar es salaam, ambazo alipopanda hazikuota akalazimika
kupanda upya.
Na Lumemo blog
Post a Comment
Post a Comment