GuidePedia

0
Mgeni rasmi Adeny Mwakyonde aliyevaa suti ya kijivu pamoja na mpambe wake alipokuwa akiingia uwanjanjani
MC  E, Mwinuka alipokuwa akifanya ushereheshwaji wakati wakumpokea mgeni rasmi
Mgeni rasmi alipokuwa anaenlekea kukaa katika meza kuu pamoja na wapambe wake.

Kundi la Comedy lilipokuwa litumbuiza katika uzinduzi wao.
Hii ndio CD iliyozinduliwa
Kiongozi wa kundi la Comedy Lusekelo Mwang'amba akisoma lisala kwa mgeni rasmi.
Mgeni Rasmi alipokuwa akijibu risala kutoka kwa msomaji
Mgeni rasmi alipokuwa akiondoka katika viwanja vya sherehe

Picha na Lumemo blog
...................................................................................................................................................................................


Vijana wametakiwa kujituma katika kufanya kazi za zakujiajiri na kujipatia kipato ili kuondokana na wimbi la umasikini linalowakabili vijana.

Hayo yamesemwa na mjumbe wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi CCM mkoa wa mbeya Adeny Mwakyonde alipokuwa katika uzinduzi wa filam ya vichekesho (COMEDY)uliyofanyika jana katika kijiji cha Lusanje kata ya mpombo halmashauri ya Busokelo iliyochezwa na kundi la msukuma Comedy.

Mwakyonde ambaye pia ni mjumbe wa mkutano mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa amesema kuwa moja kati ya ajira sahii na yauhalali ni kucheza filam kwani vijana wengi wa mijini kwa sasa wamejikita katika kuelimisha jamii kwa njia ya maigizo.

Mwakyonde ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika uzinduzi wa filam hiyo iliyojulikana kwa jina la msukuma Comedy, alilipongeza kundi hilo kwakujituma kufanya kazi yenye tija katika jamii.

Aidha Mwakyonde aliliunga mkono kundi hilo kiasi cha shilingi laki nne keshi na kuahidi kuwaongezea shilingi laki moja na kuwatafutia wadhamini sehemu mbali mbali ili kuwaendeleza vijana hao.

Nae mgeni aliyeongozana na mgeni rasmi Furaha Mwambungu amesema nijitihada nzuri walizozifaya vijana hao hivyo hana budi kuwaponmgeza kwa kazi nzuri ya kuelimisha jamii, pia amewaunga mkono kwa kiasi cha shilingi elfu hamsini na kuahidi kuwaongezea shilingi elfu hamsini nyingine siku za hivi karibuni.

Hata hivyo kiongozi wa kundi hilo  Lusekelo Mwakang’amba amesema anawashukuru watu wote waliyoitikia wito huo kwakujitokeza kwa wingi na kuwaunga mkono kwa hali na mali.

Aidha amemshukuru mgeni rasmi kwakuacha kazi zake kuja kuhudhuria uzinduzi huo na kuwaunga mkono kiasi cha shilingi laki nne keshi pamoja na mgeni aliyeongozana nae kwakuwaunga mkono kiasi cha shilingi elfu hamsini keshi.
    

Post a Comment

 
Top