GuidePedia

0
MAHAKAMA ya wilaya Nkasi mkoani Rukwa imemhukumu kwenda jela miaka miwili afisa mtendaji wa kata ya Mtenga Damas Ismail (35) kwa kosa la kumuibia mwajiri wake ambaye ni halmashauri Tshs,5050,000 ambayo yalikusanywa kama ada ya viwanja

Kwa mujibu wa mashitaka yaliosomwa mbele ya mahakama hiyo na mwendesha mashitaka wa polisi mkagaguzi msaidizi Hamimu Gwelo ni kuewa mtuhumiwa akiwa kama mtumishi wa halmashauri alimwibia mwajili wake kiasi hicho cha fedha mwaka 2011 baada ya kuhamishiwa ndani ya mamlaka ya mji mdogo wa Namanyere akitokea kata ya Mtenga

Alisema kuwa mtuhumiwa huyo kwa makusudi aliamua kuziiba fedha hizo huku akijua kuwa ni mali ya mwajili wake ambaye ni halmashauri ambapo alifanya kosa hilo katika nyakati tofauti ambapo katika mahakama hiyo alikuwa anatuhumiwa kwa makosa matano ambapo  yote alikua akimuibia mwajili wake

Hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya wilaya Nkasi Ramadhani Rugemalila baada ya kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka  pasipo kuacha shaka yoyote alimtia hatihani mtuhumiwa huyo kwa kumpeleka jela miaka miwili na akitoka atalazimika kumlipa mwajili wake kiasi hicho cha fedha Tshs,5050,000

Alisema kuwa mtuhumiwa anatiwa hatiani chini ya kifungu namba 258 na 270 sura ya 16 ya kanuni ya adhabu  iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2002

Awali upande wa mashitaka uliiomba mahakama hiyo kutoa adhabu kali kwa mtuhumiwa ili liwe ni fundisho na kwa watumishi wengine wenye nia ya kutaka kufanya kosa kama hilo,ukichukulia hivi sasa watumishi wengi wa serikali wamekuwa wakituhumiwa kufanya vitendo kama hivyo vya uhalifu.

Post a Comment

 
Top