GuidePedia

0

                       

Mgeni rasmi Aden Mwakyonde Mwambepo alipokuwa anawasili katika viwanja vya sherehe

  Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiria mali State Mwaipasi akisoma risala kwa mgeni rasmi


Mgeni rasmi akiwa katika msafara wa kukagua vyumba vya biashara.


                                     Baadhi vyumba vya biashara katika eneo hilo

Mwenyekiti wa kijiji cha mbigili Gwakisa Mwamlenga alipokuwa akimshukuru mgeni rasmi.

          Mgeni rasmi alipokuwa akienda mbele kujibu lisala ya wajasiriamali.


   Burudani za ngoma aina ya mang"oma zikiendelea katika viwanja vya sherehe



Mgeni rasmi akipewa zawadi ya mbuzi na mkungu wa ndizi na wazee wa kijiji hicho.

Mgeni rasmi alipokuwa amekaa katika kiti chake jukwaa kuu alivaa suti nyeusi hapo mbele




                                   Hii ndiyo lisala ya kikundi kwa mgeni rasmi.

 

 

Wajasiriamali wa kijiji cha mbiligili kata ya Lwangwa Halmashauri ya Busokelo Mkoani Mbeya wamepongezwa kwa juhudi zao walizozionesha katika kujenga vyumba vya maduka kwaajili ya kupangisha kama mradi wa kikundi hicho.



Pongezi hizo zilitolewa na Mjumbe wa kamati ya siasa ya chama cha Mapinduzi  (CCM) Mkoa wa Mbeya na mjumbe wa mkutano mkuu wa CCM Taifa Bw, Aden Joseph Mwakyonde Mwambepo alipoalikwa katika hafla ya uzinduzi wa vyumba hivyo uliyofanyika jana katika kijiji cha mbigili kata ya lwangwa Halmashauri ya Busokelo.




Aden Mwambepo amesema kumekuwa na vukundi vingi vya wajasiriamali vikianzishwa sehemu mbali mbali lakini mafanikio yake ni machache tofauti na kikundi kilichopo katika kijiji hicho, hivyo ana kila sababu ya kuwapongeza wanakikundi kwajuhudi zao walizozifanya katika kubuni mradi huo.




Aden Mwambepo ambae pia alikuwa mgeni rasmi  katika uzinduzi huo amewataka wanakikundi wengine ambao hawana biashara ya kufanya, wajitahidi kutafuta mitaji kwa njia halali ili waweze kufanya biashara, “kutokana na jitiada hizo mlizoenesha sina budi kuwapongeza kwa kazi nzuri na kwa wale wajasiriamali wote ambao hawajaanza kufanya biashara huu ndio wakati wao wa kufanya biasha kwa maana fursa iliyopo inatosheleaza kufanya biashara”




Aidha Adeni Mwambepo alimpongeza Prof, Mwakyusa na Mwandosya kwa kazi nzuri walizozifanya za kupeleka umeme kila sehemu ya halmashauri hiyo, kwani umeme ndiyo chachu ya maendeleo katika jamii, “ nampongeza sana Prof Mwakyusa na Mwandosya kwakutuletea umeme maana sasa tunauwezo wakufanya  biashara mpaka usiku kwasababu mwanga upo, jamani wana lwangwa tutumie fursa hiyo katika kuleta maendelo ya Halmashauri yetu”




Hata hivyo Aden Mwakyonde Mwambepo katika kuwaunga mkono wajasiriamali hao aliwachangia kiasi cha fedha taslimu shilingi milioni moja 1,000,000/= “nimefurahi sana kwakunipa heshima hii wana mbigili maana hii ni heshima ya kipekee sana, mngeweza kumpatia mtu mwingine yeyote lakini mkaona mnipatie mimi, jambo lingine nimefurahi sana kwa juhud zenu za ujenzi wa vibanda hivyo kwaiyo mimi ninawachangia fedha keshi shilingi milioni moja.




Nae mweyekiti wa kikundi hicho State Mwaipasi kwaniaba ya wanachama wake amesema anamshukuru sana mgeni rasmi Aden Mwakyonde Mwambepo kwamchango wake aliyoutoa wa fedha pamoja na kuacha kazi zake kwaajili ya kuwasikiliza katika hafla yao.
   

                                           Na, Lumemo blog










Post a Comment

 
Top