GuidePedia

0
Inline image 1

Mwenyekiti wa wenyeviti Antony Mwalugembe akitoa mrejesho
.............................................................................................

WENYEVITI wa Serikali za vijiji katika jimbo la Rungwe Magharibi Wilayani Rungwe mkoani Mbeya  wamegoma rasmi kufanya kazi za Serikali katika vijiji vyao kutokana na Serikali kupitia halmashauri ya wilaya hiyo kushindwa kuwapa stahiki zao.

Tamko hili limefanyika leo katika mkutano mkuu  ulioitishwa na wenyeviti wote wa jimbo hilo uliofanya kwenye viwanja vya shule ya msingi Bulyaga kata ya Kawetele mjini Tukuyu na kuhudhuriwa  na mamia ya wakazi wa wilaya hiyo walioonekana kuwaunga mkono wenyeviti hao.

Akizungumza katika mkutano huo Mwenyekiti wa wenyeviti  wilayani humo Anton Mwalugembe alisema kuwa siku ya tarehe 12 mwezi huu yeye pamoja na viongozi wenzake waliitwa na mkuu wa wilaya Chrispin Meela ofisini kwake kwa ajili ya kulizungumzia suala hilo huku akiwashirikisha Mkurugenzi wa halamashauri hiyo Gwabo Mwansasu,mwenyekiti wa halmashauri Mwakipiki Mwakasangula pamoja na katibu tawala na afisa utumishi.

Mwalugembe alidai kuwa mkuu wa wilaya alitaka kujua tatizo lao ambapo alimueleza kuwa wao wanataka kulipwa posho zao kwani tangu waingie madarakani miaka kumi iliyopita hawajawahi kulipwa posho  kama ilivyo agizwa bungeni, tarehe 31 agosti 2013,wala semina pamoja na serikali kutothamini mchango wao katika shughuri za maendeleo.

 Alisema baada ya maelezo hayo mkuu huyo wa wilaya aliiagiza halmashauri kusikiliza na kuyatekeleza madai ya wenyeviti kwa kuanza kuwapa semina kabla ya ushaguzi ujao na kuwataka wenyeviti kusuburi kwani suala la posho pamoja na kuwa bunge lilitangaza lakini halijaanza kutekelezwa.

Alieleza kuwa leo tarehe 14 februari 2014 alitoa mrejesho wa yale yote waliyoelezwa na mkuu wa wilaya ili wajumbe wachangie katika kuchangia wenyeviti  hao walipinga hatua hiyo na kudai kuwa hizo ni siasa hakuna kitakachofanyika.

Steven Mwakasenge mwenyekiti wa kijiji cha Iringa kata ya Ibigi alisema kuwa yeye amekuwa mwenyekiti kwa miaka 15 na anapitwa bila kupingwa kupitia CCM lakini serikali ya chama hicho imekuwa haiwajali wenyeviti wakati ndiyo wanaofanikisha shughuri zote za maendeleo katika wilaya hiyo na kuwa kuanzia leo wanasaini kufanya mgomo wa kusimama kufanya kazi katika vijiji vyao hadi pale watakapo pewa stahiki zao.

“haiwezekani sisi tufanye kazi katika mazingira magumu huku shughuri za maendeleo sikisonga mbele alafu posho wapewe maafisa watendaji pamoja na madiwani wakati wao ndiyo chachu ya maendeleo alafu wasipewe posho haiwezekani ni lazima tugome”alisema Mwakasege.

Kutokana na kauli hiyo wenyeviti wote bila kinyongo kwa hiyari yao waliandika majina yao na kuweka sahihi ya kukubari kuweka mgomo wa kutofanya kazi tena hadi pale watakapopewa stahiki zao zote maamuzi ambayo yaliungwa mkono na mamia ya wananchi walihudhuria mkutano huo.

Wananchi kwa upande wao waliwapongeza wenyeviti hao kwa ujasiri waliouonyesha wa kufanya maamuzi magumu ya kuendesha mgomo na kusema kuwa ipo haja ya Serikali wilayani humo kuliangalia kwa jicho la tatu tatizo hilo kwani linaweza likaharibu mfumo mzima wa utawala bora kwa kuwa wenyeviti ndiyo wenye watu.

Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya hiyo Gwabo Mwansasu alipofuatwa na waandishi wa habari ili kulizungumzia tatizo hilo hakuweza kuzungumza chochote.


Post a Comment

 
Top